Monday, September 14, 2009

libeneke la yale yaleeeee......

kaka Kadidi, heshima mbele mkuu!
Jumatatu ya tarehe 7 kuna mdau alituma post kulalamika kuhusu ndugu zetu wa usalama barabarani.
Napenda kutoa pongezi kwa mengi mazuri ambayo kikosi hiki kinaonekana kuyafanya katika barabara nyingi kwa siku za karibuni,Ni wazi kuwa hawa jamaa wameonyesha uwepo na uhai katika siku za karibuni kwani wanaonekana kwenye kila pembe.

PAMOJA na pongezi hizi pia kuna wengine wanaolitia doa jeshi hili! JANA (13/09/2009) nikiwa nasafiri kuelekea Iringa nilisimamishwana wanausalama barabarani maeneo ya Sanga Sanga nje kidogo na mji wa Morogoro karibu na Mzumbe, kama kawaida aliyenisimamisha alikagua kila kitu stahili katika gari ikiwemo leseni yangu, matairi,taa, insurance, m.v licence, triangle, fire extinguisher n.k,

kila kitu kilionekana kuwa safi! Askari huyu alidai chai ambayo sikuwa tayari kumpatia, ndipo akaniambia ataanza kukagua mfumo mzima wa kwenye gari , kwangu nilimwambia aendelee, katika kukagua weiper zilikuwa zinafanya kazi ila maji ndio yalikuwa hayatoki (MAJI YA WEIPER!!) jamaa akashangilia na kudai ni mojawapo ya makosa 39 yaliyoko katika NOTIFICATION TRAFIC OFFENCES hivyo akadai nimpatie nusu ya fine ambayo ni 10,000/=yaishe au nilipe fine 20,000/=,

kidogo tulishindwana lugha hapa. baada ya mabishano jamaa alingangania nilipe fine pamoja na kuwa wenzie walimsihi kuniachia na kunipa onyo!Sikuwa na jinsi ila kulipa fine ambayo ni 20,000/=.

Naomba kuuliza hivi hii ni sawa??????

je magari yote huwa yanakaguliwa hivi au ni njaa tu ya huyu jamaa?

No comments: