Saturday, September 12, 2009

mkata wafunga barabara kushinikiza kupatiwa maji bei chee
mdau pernille wa libeneke la http://pernille.typepad.com leo mchana alijikuta amekwama kwenye bonge la foleni sehemu za mkata, kiasi cha kilomita 7o hivi toka segera katika njia ya kuelekea tanga na arusha, baada ya wananchi wa hapo kufunga barabara kushinikiza mwenyekiti wao aondolewa madarakani kwa tuhuma za ufisadi. inasemekana mwenyekiti huyo alizuia mfanyabiashara mmoja wa maji ya kunywa na kumruhusu mwingine ambapo wa kwanza alikuwa anauza kwa shilingo 300/- na huyu wa mwenyekiti alikuwa akidai sh. 500. wakazuia barabara ili kufikisha ujumbe.
polisi walipofika ilibidi wafyatue risasi hewani kuutawanya umati wa watu ambao waliweza kuzuia barabara kwa zaidi ya masaa mawili. hatimaye muafaka ukafikiwa na mwenye kuuza maji bei chee akaruhusiwa kuendelea na biashara, na hatma ya mwenyekiti bado haijulikani
juu na chini ni tenka la maji ya bei poa ambalo linalakiwa kwa chereko na vifijo

















No comments: