Friday, September 4, 2009

MANDY JUMA FURAJI ATUA UINGEREZA KWA MAFUNZO YA TENNIS
Kijana Mandy akijidai na bendera ya taifa akiwa ubalozini jiini London. Chini akiwa na Balozi wetu Uingereza Mh. Mwanaidi Maajar
Mandy akiwa pamoja na Baba yake Bwana Juma
Rajabu Furaji na Bwana Hareen Wasantha, Mkurugenzi na ni Kocha wake.

Mandy akiwa na wenyeji wake
Mandy akiwa kwenye picha ya pamoja na
Mh. Balozi, wenyeji wake, baba mzazi, Kocha na Maofisa wa Ubalozi
Mandy Juma Rajabu Furaji ni kijana mdogo wa Kitanzania aliyebahatika kupata ufadhili wa kuhudhuria chuo maalum cha kufundishia mchezo wa Tennis kiitwacho Tennis Avenue Academy hapa nchini Uingereza.

Kijana Mandy akiongozana na baba yake Bwana Juma Rajabu Furaji na wenyeji wao hapa Uingereza, Bwana na Bibi Mansela, walipata nafasi ya kutembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania hapa nchini Uingereza, na kupokewa na Mheshimiwa Balozi, Mwanaidi Senare Maajar, pamoja na maofisa wengine wa Ubalozini hapo.

Baada ya kufanyiwa majaribio kadhaa na Walimu na Wataalamu wa Chuo hiko wamefurahishwa na wameridhia na kipaji, kiwango na umakini wa kijana Mandy na kumzawadia Scholarship {Ufadhili} kwa Umahili wake alionao kwenye mchezo huo maarufu wa Tennis.
Ikumbukwe kuwa mchezo huo wa Tennis ni aghari sana nchini Uingereza na kwenye nchi zilizoendelea.
Mandy ataendelea na mafunzo yake ya Tennis chini ya Kocha wake na ambaye ni Mkurugenzi wa chuo hiko cha Tennis Avenue Academy kilichopo maeneo ya New Malden Surrey Bwana Hareen Wasantha.

Unaweza kutembelea chuo hiko kwenye mtandao hapa chini:-
http://www.tennisavenue.co.uk/

No comments: