Monday, September 14, 2009

swali kwa wadau wa mwanza: nyerere wetu yuko wapi??
sanamu ya baba wa taifa iliyokuwa katika bustani
ya mnara wa saa jijini mwanza enzi hizo
sehemu iliyokuwepo sanamu ya baba wa taifa hivi sasa iko tupu. haijulikani imeenda wapi, ingawa redio mbao zinadatisha data mbali mbali. moja inasema sura ya sanamu hiyo ilikosewa hivyo imeenda kurekebishwa, ingine inadai kwamba wakuu wameiondoa sanamu hiyo baada ya kukaa bila matunzo kwa muda mrefu kiasi kwamba vinyesi vya ndege viliiharibu na kuleta taswira mbaya. wengine wanasema dili halijakaa sawa. ni matumaini wadau wa mwanza mtatupa jibu muafaka. lakini wadau watembeleao jiji hilo wanalalamika kwa kukosa kumuona mwalimu
mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
hakika wakuu wa mwanza wanajitahidi kuitunza sehemu hii muhimu
kijani cha pahala hapa kinamwagiwa na kutunzwa vyema
mandhari ni ya kuvutia ila pangenoga zaidi endapo kama baba wa taifa angerejeshwa pahala pake. wadau mnasemaje??




No comments: