Monday, August 4, 2008

Nadhani wadau mnafahamu vitanda hivi teremka tukaze, kumbe bado vipo na wananchi wanavitumia kwa saana!! mambo ya pwani hasa haya!
Nafasi za Kazi

Musoma Urban Water and Sewarage Authority
The Managing Director,Musoma Arban water and Sewarage Authority ,BOX 233, Musoma
A University Degree in Civil,Sanitary/Environment
Daily News
21/7/2008
Deadline :: 9/8/2008

UNFPA
UNFPA Representative, BOX 9182,Dar es Salaam
Advanced degree in Public health

25/7/2008
Deadline :: 10/8/2008

UNEPA
UNEPA Representative,BOX 9182,Dar es Salaam
Post Secondary Education with relevant certificate, at at least at Diploma level
Mwananchi
25/7/2008
Deadline :: 10/8/2008

DAWASCO
The Chief Executive Offer, DAWASCO. Box 5340, Dar es salaam
Graduate Engneer from a reputable university or Technician Engineer with Advanced Diploma
Mwananchi
Jul 17, 2008
Deadline :: Aug 7, 2008

DAWASCO
The Chief Executive Offer, DAWASCO. Box 5340, Dar es salaam
Full Technician Certificate (FTC) from a reputable institutions as a minimum qualifications
Mwananchi
Jul 17, 2008
Deadline :: Aug 7, 2008

DAWASCO
The Chief Executive Offer, DAWASCO. Box 5340, Dar es salaam
Degree in Chemistry from a reputable institution or Full Technician Certificate (FTC)
Mwananchi
Jul 17, 2008
Deadline :: Aug 7, 2008

The Public Procurement Reguratory Authority.
The Chief Executive Officer, The Public Procurement Reguratory Authority. Box 49. Dar es salaam
Holder of diploma in Secretarial studies from a recognised institutions
Mwananchi
17 Jul, 2008
Deadline :: 07 Aug, 2008

DAWASCO
The Chief Executive officer, DAWASCO. Box 5340, Dar es salaam.
Degree in Chemistry from a reputable institution or Full Technician Certificate (FTC)
Mwananchi
17 Jul, 2008
Deadline :: 07 Aug, 2008

DAWASCO
The Chief Executive officer, DAWASCO. Box 5340, Dar es salaam.
Full Technitian Certificate (FTC) from a reputable institutions as a minimum qualifications
Mwananchi
17 Jul, 2008
Deadline :: 07 Aug, 2008

DAWASCO
The Chief Executive officer, DAWASCO. Box 5340, Dar es salaam.
Graduate Engineer from areputable university and or Technician Engineer with Advanced Diploma
Mwananchi
17 Jul, 2008
Deadline :: 07 Aug, 2008

UCHAFU JIJINI

Yaani watu wameamua kufanya dustbin katikati ya barabara katika makutano ya Morogoro na Bibi Titi, sijui sheria gani zinaweza kutufanya watanzania tustaarabike?

Jamani hutu tu shimo kwenye barabara zetu za Dar es salaam mjini tutaisha lini, ingawa ni vidogo lakini vigumu kuvipita!
Old Is Gold!


Maggid alipotembelea makumbusho moja huko Sweden. Hivyo ni baadhi ya vitu alivyoviona.
Nashukuru sana mkuu Maggid kwa picha zako hizi!!
Rais Kikwete atembelea Mradi wa
Makaa ya Mawa wa
Mchuchuma...
Rais Jakaya Kikwete akitazama makaa ya mawe alipotembelea Mradi wa Makaa hayo ya mawe wa Mchuchuma Coal Mine Mkoani Iringa jana.
----------
Na Mgaya Kingoba,Ludewa
Rais Jakaya Kikwete jana alitembelea mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na kuwaahidi wakazi wa Ludewa na taifa kwa ujumla,kuwa dhamira ya serikali ni kuhakikisha mradi huo unakamilika katika siku za karibuni.Akihutubia wananchi baada ya kukagua mradi huo, Rais Kikwete alisema suala la mradi huo na ule wa chuma wa Liganga yamewekwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ya mwaka 2005/2010 na kwamba,masuala hayo yamekuwa ya muda mrefu,hivyo umefika wakati yatekelezwe.
Rais alisema kwa upande wa Mchuchuma, kazi ya utafiti imekamilika,anatafutwa mwekezaji na kwa Liganga utafiti unaendelea.“Kazi ya sasa ni kuona namna gani kutekeleza kazi hiyo ili tukamilishe haraka kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wa Ludewa na taifa kwa ujumla,” alisema Rais.
Alisema mradi wa Mchuchuma unatarajiwa kuzalisha tani milioni 500 na kwa upande wa Liganga ni tani 1,000,kiasi ambacho ni kikubwa na kitaleta msukumo mkubwa zaidi.
“Tulichoamua sasa ni kutafuta njia ya haraka ya kuendeleza miradi hiyo.Tatizo letu kubwa kuliko yote itakuwa namna gani ya kuhakikisha tunafikisha mazao hayo kwenye soko,” Rais Kikwete.Alisema,tatizo ni namna ya kujenga reli kutoka Mchuchuma inayotarajiwa kugharimu dola bilioni 1.6 za Marekani.
Kwa mujibu wa Rais Kikwete,suala la kujenga barabara nalo ni gumu kwa sababu njia fupi zaidi ni kilomita 70 ambayo inapita katika milima na mabonde.“Dhamira yetu sisi kama wanadamu ni kwamba tusishindwe kwa hiyo katika muda si mrefu tutakuwa tumepata jawabu na kuanza kutekeleza miradi hii,”alisema.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),Gideon Nasari alisema uchunguzi kuhusu makaa ya mawe umekamilika na kwamba hivi sasa anatafutwa mwekezaji atakayekuwa mbia katika mradi huo.Nasari alisema mradi huo,mbali na kutarajiwa kuzalisha megawati 400 za umeme,pia unatarajiwa kuyeyusha chuma cha Liganga.
Alisema nafasi kwa ajili ya wazabuni kuomba kuwekeza katika mradi huo zimeshatangazwa,na tayari kampuni 50 za kimataifa zikiwamo kutoka China,Australia,Japan,India na Afrika Kusini zimetuma maombi.Kwa mujibu wa Nasari,zinahitajika dola za Marekani milioni 800 kwa ajili ya kujenga njia ya umeme kwenda katika gridi ya taifa,dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya kujenga miundombinu na ofisi.
Awali akizungumza katika eneo la mradi,Mkomang’ombe,Rais Kikwete aliagiza kuwa taratibu zifuatwe wakati wa kuhamisha wananchi kwenye eneo la mradi,kwa kuwa kuna watu wenye maeneo yao na wameishi hapo kwa muda mrefu.
Wazee wa gwasumaa.....

Bendi ya FM academia kama kawaida usiku wa jana walipagawisha wadau mbalimbali kwenye shidano la kumtafuta Miss Vodacom Tanzania 2008 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam wakiongozwa na kiongozi wa Mkuu Nyoshi El-Sadaat wa kwanza Kulia pichani wakifanya vitu vyao jana..
Nelly Kamwele Miss Global
Publishers 2008...
Mshindi wa Shindano la Miss Global Publishers 2008 Nelly akiwa akiwa na Tabasam la nguvu muda mfupi baada ya kuvikwa taji hilo na kitita cha Tsh 500,000
Meneja Mkuu wa Global Publishers Limited Bw Abdallah Mrisho Salawi akimtangaza Mshindi wa Miss Global Publishers ambapo nafasi hiyo imechukuliwa na mrembo Nelly mabaye pia alijishindia kitita cha Tsh 500,000.usiku huu kwenye Hotel ya Movenpick jijini Dar es Salaam
Miss Tanzania 2007 Richa adhia ane alikuwepo kwenye sherehe za kumtangaza Mshindi wa Miss Global Publishers 2008.
Mshindi wa Shindano la Mis GlobalPublishers Nelly akiwa katika Pozi mwanana muda mfupi kabla ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo lilofanyika usiku huu Movenpick Hotel
jijini Dar es Salaam
Jokate Mwigolo akimvisha Nelly Taji la Miss Global Publisher 2008 Usiku huu Movenpick
Hotel jijini Dar es Salaam mara baada ya kutangazwa mshindi.
Meneja Mkuu wa Global Publishers Bw Abdallah Mrisho Salawi akimpongeza Mrembo Nelly Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji la Miss Global Publishers 2008 usiku huu Movenpick Hotel jijini Dar es Salaam.
WADAU MREMBO NELLY KAMWELE NDIYE MISS GLOBAL PUBLISHERSTZ.COM 2008 KWA MUJIBU WA KURA ZENU MLIZOZIPIGA KUPITIA MTANDAO WETU WA http://www.globalpublisherstz.com/TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUWASHUKURU WASOMAJI WETU KWA USHIRIKIANO WENU NA TUNAWAAHIDI KUENDELEA KUWALETEA VITU VIZURI ZAIDI.
ASANTANE SANA!!!!
ABDALLAH MRISHO SALAWI
MENEJA MKUU
GLOBAL PUBLISHERS LIMITED.
Jose Chameleone afanya Mambo
Miss Vodacom Tanzania
2008...
Mwanamuziki Jose Chameleone kutoka Uganda akifanya vitu vyake Usiku wa Kuamkia jana kwenye Shindano la Miss Vodacom Tanzania 2008 kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambapo Mrembo Nasreem Karim kutoka kanda ya Ziwa aliibuka Mshindi baada ya kuwashinda Warembo wenzake 26 na kutawazwa Rasmi kushika Taji hilo kwa Mwaka huu..
Rais Kikwete azindua Soko
IgagalaNjombe
Leo..
Rais Jakaya Kikwete(Kushoto)akiongea na mmoja wa wafanyabishara akina mama wa nyanya katika Soko la Igagala,Njombe,Bi Grace Shirima baada ya kufungua Soko jana .
Rais Jakaya Kikwete(Kushoto)akiangalia mboga aina ya Figiri muda mfupi baada ya kufungua soko La Igagala Njombe,iringa jana.Picha na Freddy Maro/ikulu