Monday, August 4, 2008

Rais Kikwete azindua Ujenzi wa
Sekondari Njombe..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kwenye jiwe la Msingi ili kuzindua ujenzi wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Anna Makinda katika kijiji cha Kilocha,wilaya ya Njombe wiki iliyopita.Picha hii ni ya Freddy Maro/ikulu
Nasreem Karim Miss Vodacom
Tanzania 2008...
Miss Vodacom Tanzania 2008 nasreem Karim akifurahia ushindi na mshindi wa pili Sylvia Mashuda(shoto) na wa Tatu Pendo Laizer muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa Mwaka huu.
Kimwana Syvia Mashuda alichaguliwa kuwa Miss TACAIDS 2008
Miss Tanzania 2007 Richa adhia akitoa shukrani zake kwa wadau mbalimbali baada ya kumaliza kipindi chake usiku wa jana na kukabidhi Taji hilo la Miss Tanzania 2008 kwa Nasreem Karim.
Miss Tanzania 2007 Richa adhia akisubiri kutangazwa kwa mshindi wa Shindano
hilo kwa Mwaka huu
Miss Tanzania 2008 Nasreem (Kati)akiwa na Mshindi wa pili Pendo David(kushoto)
na wa Tatu Sylvia Mashuda.
Miss Tanzania 2008 Nasreem Karim akiwa ndani ya gari lake baada ya kukabidhiwa kwenye fainali za Vodacom Miss Tanzania 2008 viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.
Majaji wa Miss Tanzania 2008 wakijumlisha kura muda mchache kabla ya kutangaza
Mshindi wa Taji hilo usiku wa kuamkia jana kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam

Kikwangua anga Cha Nguvu
Chaja Bongo...
Jengo la Uhuru Heights limesanifiwa kuwa jengo refu nchini mahsusi kwa ajili ya biashara na makazi.Kivutio hicho cha jengo kimebeba nembo ya mwenge wa uhuru ambao uliwekwa kwenye kilele cha Mlima KilimanjaroJengo hilo la Uhuru Heights ni mradi muhimu kwa ajili ya kuifanya mitaji ya biashara na lipo sehemu nzuri kwenye Barabara ya Bibi Titi Mohammed katikati ya jji eneo la Upanga na OysterBay.

Jengo hili litajengwa mbele ya bahari na litaweza kutoa fursa kwa watu kutazama na kupata upepo wa bahari ya Hindi na litakuwa na vifaa vilivyotengenezwa kwa ubora unaokubaliaka duniani.Eneo litakapojengwa ni zuri na litavutia kibiashara.Ghorofa tano ndani ya jengo zitakuwa ni kwa ajili ya ofisi zenye ukubwa tofauti.Usanifu wa jengo na umaliziaji wa hali ya juu kutawezesha na kukidhi uendeshaji wa shughuli kama vile kuunganishwa na Intaneti iliyo na kasi kubwa,maegesho na ulinzi kwa saa 2.

Jengo hili litakuwa na ghorofa 25 litakuwa ni eneo la kuvutia,likiwa na burudani na mambo mengine ya kuvutia katika maisha ya jamii.Duka la nguo za mitindo ya aina mbalimbali litakuwa kwenye mwanzo wa jengo chini na kwenye ghorofa ya kwanza na litaonyesha mitindo mbalimbali inayopongoza kwa ubora duniani.Ghorofa ya pili itakuwa na mgahawa ambao utakuwa ni wa kipekee utakaokuwa na mchanganyiko wa vyakula kutoka tamaduni mbalimbali na utahudumia wateja kutoka mataifa mbalimbali sanjari na ukumbi mkubwa wa chakula.

Ukumbi wa burudani utakuwa na eneo la michezo mbalimbali ya watoto na ukumbi wa michezo.Kwenye maeneo ya makazi ya jengo hilo kutakuwa na bwawa la kuogelea na sehemu ya kufanyia mazoezi ya viungo(gym)kwa ajili ya wanawake na wanaume,eneo lamichezo kwa ajili ya watoto na ukumbi wa sherehe ambao unaweza kuchukua watu 100 hadi 120.Habari zaidi zinakuja..

Saturday, August 2, 2008

MHH hapa je ? ..

katika pita pita zangu nikakutana na ujumbe wa dizaini hii wadau huyu jamaa mwenye hii gari tumueleweje lakini !!
Rais Kikwete azindua Ujenzi wa
Sekondari Njombe..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kwenye jiwe la Msingi ili kuzindua ujenzi wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Anna Makinda katika kijiji cha Kilocha,wilaya ya Njombe jana.Picha hii ni ya Freddy Maro/ikulu

Wanafunzi wakiandamana Dar JANA kupinga ongezeko la nauli.
Waliziba hata barabara kupinga ongezeko hilo na waliimba nyimbo za kimapambano kuonyesha kilio chao.
Hawakuogopa mabomu wala bunduki walikuwa ngangali kinoma.
Walibeba mabango yenye ujumbe wa kutisha!
Baadae walijua kuwa vyombo vya dola vina nguvu wakakwepa yasitokee ya Soweto!

Wanafunzi wakimkoromea polisi aliyekuwa ndani ya gari na akiacha makondakta wawazuie kupanda na kumshutumu kuwa anauchuna kwa kuwa yeye anapanda bure!!!! Bado kidogo wamtoe macho.
Rais Karume akutana na
Masha..
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK AMANI ABEID KARUME(KUSHOTO),AKISALIMIANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MH LAURENCE KEGO MASHA,ALIYEFIKA IKULU MJINI ZANIBAR KUONANA NA RAIS JANA.PICHA NA RAMADHAN OTHMAN IKULU/ZANZIBAR
Kampuni ya Celtel sasa Kuitwa
Zain...
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Simu za Mkononi ya Zain(zamani Celtel)kwa Kanda ya Afrika Mashariki,Bashar Arafeh akizungumza na waandishi Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa jina hilo.
------
Kampuni ya simu za mikononi ya Celtel imebadilisha jina la biashara na kuanzia jana,inajulikana kama Zain.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Zain Kanda ya Afrika Mashariki,Bashar Arafeh alisema hatua hiyo pia inakwenda sambamba na kuunganishwa mabara mawili kwa mtandao mmoja.

“Kuibadilisha Celtel kuwa Zain ni mwanzo wa enzi mpya kwa wateja wa Celtel nchini Tanzania. Lengo ni kuwa kampuni ambayo inahudumia duniani kote,na baada ya mwaka 2011 kuwa miongoni mwa kampuni 10 bora duniani,”alisema.Arafeh alisema mabadiliko hayo haya athiri masuala ya hisa.Alisema serikali inaendelea kumiliki hisa asilimia 40 na asilimia 60 zitabaki kwa Zain.

Kwa mujibu wa Arafeh,kampuni hiyo ambayo ina miaka 10 tangu ianzishwe,imekuwa ikitoa huduma katika nchi 14 za Afrika na kwamba itaongeza huduma na kufikia nchi 15 mwisho wa mwaka huu.Habari na Anastazia Anyimike.Picha Mrock
Leo Ndio Leo....
LEO NDIYO LEO,ASEMAYE KESHO MUONGO.
Leaders Club pako tayari kuwapokea warembo wote katika jukwaa la kisasa.Bila kusahau mchuano wa kumtafuta Miss Global Publisherstz.com unaendelea..piga kura Hapa kumchagua mrembo wa kuondoka na kitita cha shilingi 500,000