Tuesday, December 27, 2011

MATUNDA YA LEMA YAANZA KUONEKANA WORLD BANK WAHOJI MATUMIZI MAKUBWA ARUSHA



SAKATAla ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, limeingia katika hatua nyingine baada ya Benki ya Dunia nchini, kutaka maelezo ya kina vinginevyo itasitisha kuendelea kutoa misaada katika Jiji hilo baada ya kubaini fedha zaidi ya Sh milioni 100 kutumika kukarabati ofisi nne za Jiji hilo.
Vyanzo vya habari kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha vilisema kuwa fedha hizo ambazo katika mradi wa benki hiyo ujulikanao kwa jina la Tanzania Strategic Cities Programmes (TSCP) wa Jiji hilo, zimetumika kukarabati ofisi za Mkurugenzi, Biashara, Mchumi na Mhandisi.

Habari za uhakika zilieleza kuwa kutumika “hovyo hovyo” kwa mamilioni hayo ya fedha, hakukuridhisha uongozi wa Benki ya Dunia kwani ulieleza kuwa ni matumizi mabaya ya fedha hivyo walitaka maelezo ya kina kwa maandishi.

Uongozi huo wa benki ulimwandikia pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo juu yahali hiyo na uamuzi ambao ofisi hiyo inataka kuchukua, ndipo mkuu huyo alipoingilia kati nakuiahidi Benki ya Dunia kuwa itafuatilia na kama kuna ulaji, hatua kali zitachukuliwa.

Habari zilieleza kuwa baada ya ahadi hiyo, ndipo benki hiyo iliamua kuacha kwanza hatua yakehiyo mpaka watakapopata taarifa rasmi ya hatua za kuchukuliwa wahusika wa ubadhilifu wa fedha hizo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Estomih Chang’a alipoulizwa juu ya kiasi hicho kutumika kukarabati ofisi nne tu, alisema taratibu zote za kutangaza zabuni zilitumika hivyo kampuni iliyofanya kazi hiyo ilipewa kazi hiyo kwa uamuzi wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi ya Jiji hilo.

Chang’a alisema kazi ya kukarabati ofisi ilitangazwa zabuni, ikafanyiwa tathmini, ikapita zabunina kuzingatiwa Sheria ya Manunuzi ya Umma kwa asilimia 100 na kama kuna lingine liko tofauti, aulizwe Mhandisi wa Jiji.

Alipobanwa ili atoe ufafanuzi iweje yeye kama kiongozi wa Jiji la Arusha na Mdhibiti Mkuu wa matumizi ya fedha, akubali kiasi hicho kikubwa cha fedha kutumika kukarabati ofisi mbili, alisisitiza aulizwe Mhandisi huyo kwa madai ndiye aliyefanya tathmini ya awali kabla ya utangazaji zabuni.

Mhandisi wa Jiji, Afwilile Lamsy alipoulizwa kwa njia ya simu, alisema na kupingana na Mkurugenzi wake kwa kueleza kuwa ofisi zilizofanyiwa ukarabati ni zaidi ya 10, hatua iliyoonekana kupingana na baadhi ya nyaraka zinazoonesha kuwa ukarabati huo ulifanywa kwaofisi nne tu.

Lamsy alisema akiwa ni mtendaji na msimamizi mkuu wa shughuli zote za ujenzi, anachojuani kuwa ofisi zilizofanyiwa ukarabati ni zaidi ya 10, lakini alishindwa kufafanua kama bajeti yake iliruhusu kampuni kutenda kwa zaidi ya Sh milioni 100 kukarabati ofisi hizo.

Mkuu wa Mkoa, Mulongo alipoulizwa kama anajua chochote juu ya utata wa matumizi ya fedhaza mradi huo, alikiri kuufahamu na kueleza kuwa kutumika kwa fedha hizo ni moja ya kazi za mradi huo.

Ila alienda mbali zaidi na kueleza kwamba tatizo ni kiasi hicho cha fedha na ndio maana Tume imeundwa kuchunguza.

“Kukarabati ofisi ni moja ya package (sehemu) ya mradi huo, lakini kuna tatizo katika utoaji wazabuni kwa kampuni kwa fedha hizo nyingi na ndio maana Tume ya Bodi ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) inachunguza kubaini ukweli,” alisema Mkuu wa Mkoa.

Source::HabariLeo::

No comments: