Monday, November 24, 2008

WANAUME TMK watoa msaada hospitali ya sokoine

Mganga mfawidhi wa hospitali ya Sokoine ya mjini Lindi Edga Mlawa akimpa mkono wa asante msanii wa kundi la Wanaume TMK Kr-Mulla kwa msaada wao walioutoa ndani ya hospitali hiyo hasa kwenye wodi ya watoto na wazazi
Msanii wa kundi la Wanaume TMK Chege Chigunda a.k.a mtoto wa mama Saidi akimkabidhi mama mzazi kwenye wodi ya wazazi baadhi ya vitu kama uonavyo pichani

Meneja wa kundi la TMK wanaume Mkubwa Said Fella akipeana mkono wa asante kutoka kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya Sokoine iliopo Mjini Lindi bw.Edga Mlawa baada ya kundi hilo kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye wodi ya watoto na wazazi,vitu hivyo kadha wa kadha zikiwemo nepi ,poda/uji wa ulezi/Lishe na vinginevyo.Kundi la TMK Wanaume walikwenda kanda ya kusini kwa ziara ya kimuziki.
Inawezekana:ama hakika huu ni mfano mzuri na wa kuigwa kabisa hata kwa makundi mengine wakiwemo wasanii solo,tusiishie kufanya mambo ya starehe,anasa na mambo mengine ambayo kimsingi hayana manufaa yoyote, kuna wakati inatupasa kuwakumbuka wenye shida hata kwa kutoa kidogo ulichonacho,WANAUME TMK SALUTE!

No comments: