Friday, November 14, 2008

Wamarekani Wamemchagua Mbabe Wa Akili

Na Maggid Mjengwa,

BENJAMIN Disraeli alipata kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza. Hapa tutamkumbuka kwa kauli yake ifuatayo; "A good leader knows himself and the times". Kwamba kiongozi mzuri hujijua na hujua wakati unaomzunguka. Hapa ina maana uwezo wa kiongozi kusoma kinachoitwa ' alama za nyakati'. Ni dhahiri kuwa zimepita zama zile ambazo mtu alikwenda shule miaka 16 au 20 kisha akatoka huko akidai kuwa ' amesoma' sana. Naam. Amesoma mpaka amefika mahali pameandikwa 'No Class Ahead! ( hakuna darasa mbele!)

Kwamba tayari mtu huyo ameshapata maarifa ya kutosha ya kuendesha maisha yake. Kama katika dunia hii bado kuna mtu anafikiri hivyo, basi, mtu huyo ana 'fikra za kizamani', amepitwa na wakati. Soma zaidi: http://raiamwema.co.tz

No comments: