
Kumradhi wadau,leo jioni nimefanya uchunguzi wangu usio rasmi katika jengo la NIC a.k.a Kitega Uchumi lenye jumla ya ghorofa 14 lililopo mtaa wa samora,jijini dar na kubaini baadhi ya uharibifu/ubovu wa hivyo viswichi uvionavyo pichani,ambavyo vipo kila ghorofa kwa ajili ya kusaidia kupambana ama kutoa taarifa iwapo kuna hitilafu yoyote ile ikiwemo ya moto iwapo itatokea.Cha kushangaza swichi zote hizo zimekufa na wahusika wameuchuna kimyaa kama vile hawajui lolote,mbaya zaidi jengo hili limewahi kuungua moto mara kadhaa kwa hitilafu za umeme na kusababisha hasara kubwa ya mali na ofisi za wapangaji wa jengo hilo. Picha hizo ni kuanzia ghorofa ya kwanza mpaka ghorofa ya 5.
No comments:
Post a Comment