Kesi Ya  Ajali Ya Wangwe Kuanza Okt 7
Mallya ambaye alifikishwa tena  mahakamani jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Thomas  Simba, aliieleza mahakama kuwa haelewi chochote kuhusiana na dhamana yake kwa  kuwa yeye yuko rumande. “Mheshimiwa Hakimu kwa kuwa nipo ndani sijui chochote  kinachoendelea kuhusiana na dhamana yangu,” alisema Mallya mahakamani  hapo.
 Alieleza hayo mara baada ya  kuulizwa na Hakimu mbele ya Mwendesha Mashitaka Mrakibu Msaidizi wa Polisi  Polycarp Urio ni nini kinachoendelea kuhusiana na dhamana yake kwa kuwa ipo  wazi. Awali alijitokeza mtu mmoja ambaye jina lake halikufahamika na mahali  alipotoka na kusema kuwa angewasilisha hati ya nyumba baada ya mahakama  kuahirishwa, lakini baada ya kumalizika kwa kesi zote mahakamani hapo, mtu huyo  hakuwa na barua ya utambulisho wala hati ya nyumba. Mdhamini anayetakiwa  kumdhamini Mallya ni mkazi wa Dodoma, mwenye barua ya uthibitisho kutoka kwa  viongozi wa eneo analoishi na dhamana ya Sh milioni tano au mali yoyote  isiyohamishika yenye thamani hiyo.Mallya anakabiliwa na shitaka la kuendesha  gari bila leseni, kwa mwendo kasi na kusababisha kifo cha Wangwe.
Habari Kwa Hisani Ya Habarileo
 Habari Kwa Hisani Ya Habarileo
No comments:
Post a Comment