

 kwa kile kinachoonekana kushindwa gemu inasemekana kuna baadhi ya  mahasimu wa kampuni ya kilaji nchini TBL wamekuwa wakiihujumu kwa kufuta  matangazo ya biashara kwenye sehemu kadhaa nchini, hasa mjini moshi na a-taun  kama inavyoonekana kwenye picha hizi zilizoletwa na mdau wa huko. kitendo hiki  haramu na cha aibu kimelaaniwa sio tu na TBL bali pia walaji wa bidhaa zake  ambao kwa hasira wamesema wataendeleza libeneke na TBL hadi kieleweke. wamedai  kuwa mtu ukishindwa gemu hii tafuta mbinu ingine na sio hujuma
   
No comments:
Post a Comment