Tumeunda Kamati Kutafuta  
 Viongozi  anaotaka  Kukihujumu
 Chama-Dr  Slaa...
  
 Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbrod Slaa akizungumza na waandishi wa  habari Makao Makuu ya chama hicho Dar es Salaam jumamosi.Kulia ni Balozi  Christopher Ngaiza.Picha na Mdau Bernard Rwebangira-----------
 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeunda Kamati  Ndogo kwa ajili ya kuchunguza viongozi na wanachama wanaotuhumiwa  kukihujumu,imefahamika.Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Wilbroad Slaa alisema hayo  jumamosi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu  tamko la Kamati Kuu ya chama hicho baada ya mkutano wake uliofanyika hivi  karibuni. 
  Dk.Slaa alisema kwa muda sasa kumekuwa na mikakati inayofanywa  na baadhi ya watu ndani na nje ya chama hicho kwa lengo la kuhujumu taswira ya  chama hicho na Mwenyekiti wake wa Taifa,Freeman Mbowe.Alisema hujuma hizo ndani  ya chama zimekuwa zikihusisha baadhi ya viongozi wa chama hicho katika maeneo  mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji kwa umma.Bofya na Endelea....>>>>>>>>>  
 
No comments:
Post a Comment