Nini  hasa hutokea wakati wa kufa?
 
 Utata wa  hisia na nini hutokea ama huendelea katika akili na mwili mtu anayeeleka kufa  unaweza kuelekea kupata ufumbuzi baada ya kuanzishwa kwa mchakato wa uchunguzi  wa miaka mitatu unaotarajiwa kuhusisha takriban watu 1500 waliokuwa katika hali  ya "nusu ufu" (cardiac arrest) kueleza hisia hizo.Uchunguzi huo utakaoongozwa na  mmoja wa wataalamu wanaotambulika duniani kwa uchunguzi wa masuala ya vifo Dr  Sam Parnia kutoka Weill Cornell Medical Center iliyoko New York nchini Marekani,  akishirikiana na wataalamu wenzake wa mradi aliouasisi na anaouongoza  unaojulikana kama Human Consciousness Project utahusisha vituo vikuu vya afya  zaidi ya 25 kutoka nchi za Ulaya, Canada na Marekani ukiwa na jina la AWARE na  kuchimba zaidi hisia za kibaolojia juu ya kile kilichoitwa "out-of-body  experience.Dr Parnia amehojiwa na jarida la TIME na kueleza mambo mengi yakiwemo  utata wa mapingamizi juu ya uchunguzi kama huo, mahojiano yake na mtu wa kwanza  kudai kuwa katika hali hiyo, changamoto za kiteknolojia kuhusiana na kile  kinachotokea wakati huo na hata njia zitakazotumika kuhakikisha yale  yatakayovumbiliwa na uchunguzi huo kwa jamii na waweza kusoma yote kwa  kubofya http://www.time.com/time/healtharticle/0,8599,1842627,00.html. Baadhi ya watu waliosoma habari  za uchunguzi wake wameshaanza kujitokeza kuhojiwa ili kuelezea yaliyowasibu ama  waliyopitia wakati wa "u-nusu ufu" huo http://answers.yahoo.com/question/index?qid=20080924095843AAYJVP9  .
 Pia waweza kupata wasifu wa Dr  Parnia kwa kubofya http://www.mindbodysymposium.com/Speakers-Panelists/sam-parnia-md-phd-mrcp.html  
 
No comments:
Post a Comment