Bomoa  Bomoa Magomeni...



 Familia sita zimekosa sehemu  ya kuishi baada ya watu wanaodaiwa kununua nyumba ya urithi ya watoto zaidi ya  10 wa marehemu mzee Yussuf Mbonde iliyoko magomeni mwembechai kubomoa nyumba  hiyo kwa kutumia greda huku wakilindwa na vijana wa kukodi maarufu wanaojulikana  kama mabaunsa pamoja na usimamizi wa polisi waliokuwa na  silaha.Bomoa bomoa hiyo ilitokea  juzi majira ya saa 9.00 alasiri baada ya uvamizi huo kutokea kusambaratisha  nyumba na vitu vyote vilivyokuwemo ndani.
Pichani juu ni baadhi ya  wanafamilia hao wakilia kwa uchungu baada ya kuona nyumba yao ikisambaratishwa  vibaya sana na vitu vyao vyote vya ndani vikiwemo...picha kwa hisani ya mzee wa  mshitu.
 
No comments:
Post a Comment