Wednesday, May 21, 2008

Habari zisizo Rasmi...


Wadau nimepokea mail mbalimbali kutoka kwa wadau wa blog hii kutaka kupata uhakika juu ya habari zilizotangazwa na baadhi ya Vyombo vya habari kuwa aliyekua gavana wa benki kuu ya Tanzania Mh Balali Daudi Balali amefariki Dunia nchini Marekani kama wengi wao walivyonukuu habari hii kutoka gazeti la Tanzania Daima Toleo la leo ambazo si rasmi.Blog hii inafanya juu chini kupata uhakika wa habari hiii na pindi mambo yakiwa Tayari tutamwaga Habari Mvunjiko kama kawaida.
------------
Mr. Kichwabuta mwendantwala - Washington DC, USA
Anasema:
Bwana Kadidi, ni KWELI kabisa huyu Bwana aitwaye Daudi T. S. Ballali (Gavana wa Zamani wa Benki kuu ya Tanzania) hatunaye tena kwani kesha FARIKI. Kwa habari zenye uhakika toka kwa ndugu wa karibu na mkewe, Mama Anna Muganda zinatonya kuwa amefariki tarehe 16.05.2008 huko BOSTON, USA. Na mipango ya mazishi inafanywa kwa ndugu na jamaa wa marehemu na Taarifa zaidi tutakutumia mara tu tutakapopata habari zenye uhakika.R.I.P. Mr. Daud Timoth S. Ballali (Ex-Governor, Bank of Tanzania)

No comments: