Sunday, September 7, 2008

Mzee Lowassa,Nape Kujadiliwa
Wiki Ijayo.

Mbunge wa Monduli/Waziri Mkuu aliyejiuzulu Mheshimiwa Edward Lowassa.
-----
KIKAO cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),kimeweka kiporo baadhi ya ajenda zake nyeti,ikiwamo ile inayogusia suala lenye utata la mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Umoja wake wa Vijana(UVCCM),ambalo linatishia umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi wa CCM.

Hoja ya mradi huo,iliyoibuliwa na mwanasiasa chipukizi ndani ya UVCCM,Nape Nnauye, anayewatuhumu Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la UVCCM,Edward Lowassa,Mwenyekiti wa umoja huo anayemaliza muda wake,Dk.Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo,Francis Isaac,kwa kuiingiza jumuiya yao katika mradi usio na tija wala masilahi kwao.

Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho cha CC kilichokutana juzi zinaeleza kwamba,suala hilo sasa linatarajiwa kujadiliwa Jumanne ijayo na uamuzi kuhusu mradi huo mzima utafikiwa kabla ya mapendekezo ya Kamati Kuu kupelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho tawala(NEC),kwa maamuzi siku hiyo hiyo.Bofya na Endelea...>>>>>>

No comments: