Jacob Zuma atembelea Chua Kikuu
Cha Kilimo(SUA)...
------
Rais wa chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress(ANC),Jacob Zuma amesema kama kuna nchi moja duniani iliyochangia zaidi kuliko nyingine yoyote duniani kuleta uhuru wa Afrika Kusini na nchi nyingine za kusini mwa Afrika ni Tanzania.
Zuma amesema kwa sababu hiyo kamwe Afrika Kusini haitapata namna ya kutosha kuishukuru Tanzania kwa mchango wake usiokuwa na kifani wala mfano katika kutafuta uhuru wa Afrika Kusini na nchi nyingine za Kusini mwa Afrika.“Nchi zetu mbili zina uhusiano usioweza kukatika kwa sababu vijana wetu,watu wetu,makada wetu wamezikwa katika ardhi ya Tanzania,”alisema Zuma juzi usiku.Bofya na Endelea...>>>>>>
No comments:
Post a Comment