Ikulu Yatoa Tamko Rasmi  juu ya 
 Hosea  na Mwanyika...
Pichani ni Katibu Mkuu Kiongozi Bw Phillemon Luhanjo
 --
 Na Said Mwishehe na Reuben Kagaruki.
  SIKU chache Bungeni taarifa ya Serikali juu ya utekelezaji wa  maazimio 23 ya Bunge kufuatia kashfa ya kampuni tata ya Richmond na kubainisha  kuwa vigogo kadhaa Serikali waliohusishwa na kashfa hiyo hatIma yao iko ngazi za  juu,Ikulu imetoa tamko rasmi.
    Miongoni mwa vigogo ambao Bunge liliarifiwa kuwa majaliwa ya  ajira zao yako mikononi mwa aidha Rais Jakaya Kikwete mwenyewe au Katibu  Kiongozi Ikulu,Bw.Phillemon Luhanjo ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na  Kupambana na Rushwa(TAKUKURU),Dkt.Edward Hosea,Mwanasheria Mkuu,Bw.Johnson  Mwanyika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,Bw.Arthur Mwakapugi.  
    Ikulu jana imetoa msimamo wake kwa mara ya kwanza juu ya  kinachoendelea baada ya kuachiwa dhamana ya uamuzi juu ya vigogo hao.Akizungumza  jijini Dar es Salaam,Bw.Luhanjo(Pichani)alisema Serikali haitaki kukurupuka juu  ya hatima ya akina Hosea,Mwanyika na Mwakapugi akisema ni suala zito linalogusa  maisha ya watu na familia zao.
   "Suala hili tunalishughulikia,unaposhughulikia maisha ya mtu  haustahili kutoa uamuzi wakukurupuka..tunashughulikia,hatukurupuki,"alisema na  kuashiria kuwa kwa sasa kazi iliyoko mbele yao ni kupima uzito na athari za kila  uamuzi utakaofanyika Kabla ya kutoa uamuzi lazima upime kwanza na sio  kukurupuka..
  Hebu fikiria ungekuwa wewe mtu anakuhukumu kufungwa kwa  kukurupuka,familia yako na wewe mwenyewe mtaathirika kwa kiasi gani?alihoji.  
 
No comments:
Post a Comment