Saturday, February 13, 2010

WIZI WA MAGARI MLIMANI CITY
Kaka kadidi pole kwa libeneke.

Mie ni mdau wa blog ya . Napenda kuishirikisha jamii na kuisisitiza iwe makini wanapokuja sokoni hapa Mlimani City jijini Dar. Tayari mwanajamii mmoja akiwa anapata huduma gari yake iliibwa katika parking za hapa Mlimani City. Wakati anatoka ndiyo anaona gari inakata kona kuelekea Sam Nujoma Road na haikuwa rahisi kuiserve.

Nimejiuliza jamani hivi VIJIKADI tunavyopewa tunapoingia humu sokoni kumbe havina msaada hata kidogo. Basi ni vyema uongozi wa humu uweke vibao vya 'PARKING AT YOUR OWN RISK' ili kieleweke maana hata hawa askari wao naona hawasaidii kitu. Wametanda kila mahali kazi yao nini basi?

Imeniuma sana na sidhani kama hii kampuni ya ulinzi hapa inamsaada wowote kwa hili. Wawekee wadau kaka ili kuwapa angalisho.

Ni mimi Mdau.

No comments: