Thursday, February 25, 2010

MAULID IJUMAA USIKU, JUMAMOSI MAPUMZIKO
SHEREHE ZA MAULID ZINAZOADHIMISHWA KUSHEREHEKEA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD S.A.W ZITAFANYIKA KITAIFA MKOANI MTWARA IJUMAA USIKU WA FEBRUARI 26, 2010 MKOANI MTWARA, KWA MUJIBU WA TAARIFA KUTOKA MAKAO MAKUU YA BARAZA KUU LA WAISLAMU (BAKWATA).
KAMA ILIVYO ADA, JUMAMOSI FEBRUARI 27, 2010 SAWA NA MWEZI WA 12 MFUNGO 6, ITAKUWA NI SIKU YA MAPUMZIKO NCHI NZIMA. KATIKA TAARIFA HIYO BAKWATA LIMEWATAKIA WANANCHI WOTE MAPUMZIKO MEMA

No comments: