Kunafanana na kushikiwa akili
Huu ndio ukweli hata mkibisha, vijana wengi hasa ambao wako nje ya ndoa hukwamishwa sana na wazazi wao kufanya mikakati ya mbele na wezi wao wa maisha kutokana na ukweli kwamba wazazi wengi huhisi kwamba vijana kujiamulia mambo yao, ni utamaduni wa kigeni. Wazee wanaamini kwamba kujiamulia mambo, unatakiwa kufanya baada ya kuondoka nyumbani, suala ambalo kwa maisha ya sasa si kweli kabisa.
Wasichana wengi mno wamekatazwa hata kuionja ladha ya maisha, wazee wanasahau kwamba msichana atakapoyaanza maisha mwenyewe, hata hapo baadaye akija kuingia katika ndoa, anakuwa sio mgeni wa mambo fulani fulani ya kimaisha na huyu anakuwa si rahisi hata kuyumbishwa kimaisha na mumewe, hii dhana ya kuyumbishwa na mwanaume inakuja kwa sababu vijana wa kiume huruhusiwa kuishi peke yao hata kabla hawajaoa, kwa hiyo wanapoingia kwenye ndoa wanakuwa wana uzoefu zaidi wa maisha kuliko mtoto wa kike.
...sasa hapa kuna kitu kama kunyanyapaliwa, umeona?
Inadaiwa kwamba, kinadada wakianza maisha peke yao wanakuwa wanakimbilia sana ngono kuliko kitu kingine chochote na ni rahisi sana kuanza kuharibikiwa, hivi jamani ni kweli?
Hapa ndipo uhuru unapoanza kukosekana, utakuta watu ni wapenzi, unamwambia mwenzako jinsi ya kuanza mipango ya kimaisha lakini jibu lake lazima linakuwa kwamba ni lazima akamuulize baba au mama, na mwisho wa yote lazima jibu litakuwa Hapana!
Au utakuta kijana wa miaka 26 anapangiwa msichana wa kuongozana naye katika maisha, utafikiri hana moyo vile, matokeo ya mambo haya ndugu zangu ndio ndoa zisizodumu na mambo mengine mengi ambayo huja kwa sababu tu, vijana wanakuwa wanafanya kwa sababu baba kasema, lakini moyo wake haupendi.
Kuna mambo mengi mnajua? lakini haya ni baadhi na nimesema hivi kwa makusudi ili na wengine msiosema mpate kusema.Kijana anatakiwa kuwa na uhuru wa kujiamulia lakini pia uhuru wenyewe tuangalie.
Usipowasikiliza pia ni tatizo
Sijaandika hii ili muwe wakaidi jamani wapendanao, nimeandika hili ili tujifikirie mara mbili na tuweze kushawishi pale ambapo inawezekana ili mwisho wa siku hata kama umefanya kitu kwa kulazimishwa unaweza kwa asilimia fulani kukipunguza makali. Kukataa ya mkuu, guu linaweza kuvunjika muda wowote ule!
Kaa nao chini ujadili nao na ikiwezekana uwaelimishe kwamba hiki na hiki sio sawa, na sababu zake ni hizi, na hizi na zile, mwisho wa siku unakuta wanakuelewa, wanakwenda katika mstari ambao wewe unafikiria kwamba ni mwema.
Umeona bwana, kwa sababu wao wametutangulia, sio watu wa kuwapuuzia ile moja kwa moja ingawa nao kuna wakati wanazidi!
Kuna mambo mengi ambayo kwa sasa yamepitwa na wakati, kama Mila fulani hivi, amri amri za lazima uchukue kwa mzee fulani kwa sababu ni rafiki wa baba, na mambo mengine na sio yote upinge, kwa sababu tu, kakwambia mzee, hiyo hapana..
Naomba leo niishie hapa, nimefupisha mjadala ni mrefu na mpana lakininimeandika kwa ufupi ili tupate mawazo kutoka kwa watu sana na sio mimi. Sawa ndugu zangu?
No comments:
Post a Comment