Wednesday, March 12, 2008

Roho ya kwanini, ya nini lakini!?

Haya jamani, ..hii ni Jumatano nyingine, naomba niwakaribishe tena kwenye hii blog yetu !

Niko sehemu kwa washikaji,napumzika kidogo, mara kidogo nasikia redio redio iko ON. nasiki huu wimbo wa Christa Bella wa Akudo sound. Napoteza mawasiliano kwa muda nikiwa nausikiliza kwa makini.

Mistari ya wimbo huo: "Ukisikia nimekufa usiweke msiba.

. ila sherehekea kwa sababu una roho mbaya..." "....jifunze kusamehe, itakusaidia maishaniiiii," wimbo umenigusa sio siri.

Akilini napata wazo, kuna kitu cha kuzungumza hapa leo.

Ni ukweli usiopingika kuwa; Unapoamua kumfanyia mwenzio jambo baya unasahau kufikiria kuwa hata wewe ukifanyiwa utaumia.

Shoga nataka nikueleze wazi kuwa roho mbaya hailipi, Unabisha?

Sikia.

1. Mkuki kwa nguruwe....si ndio!

Msemo huu una maana nyingi lakini lengo lake kubwa ni kueleza vile ambavyo inauma ukitendewa mambo ambayo umemtendea mwingine ila wewe binafsi usingependa kufanyiwa. Maishani ya raha ni kuwatendea wengine yaliyo mema, yaliyo ya haki, uwajibu wengine vile ambavyo kama wewe utajibiwa hivyo utajisikia raha. Sasa hivyo hivyo ni katika mabaya. Using'ake utakapotendwa na wewe kama ulivyomtendea mwenzako.

2. Umesahau, What goes around....!

Kwa ujumla ninachotaka kuzungumzia katika makala hii leo ni kuhakikisha unawatendea wenzi wako mambo yaliyo mema, mambo ambayo kwa hakika wewe ukifanyiwa utajisikia raha. Ni kama nilivyosema, ukimfanyia mwenzako mabaya ujue hata wewe utafanyiwa. Kama wewe si mwepesi wa kusamehe basi hata wewe hutasamehewa. Na mara nyingi jiweke wakumuombea mwenzako mema. Kwa kuwa hata wewe watu watakuombea mema vilevile.

4. `Kumbuka, Hutoishi milele...!

Katika maisha ni jambo la msingi kuhakikisha wote unawatendea yaliyo ya haki, maana hapa duniani tunapita, yanini kufanyiana roho mbaya, kwani wewe utaishi milele na hata kama, wapo wanaomini kila kitu hulipwa hapa hapa, kesho akhera ni hesabu tu.Wasomaji mnapaswa kujifunza tabia njema, unapaswa kujua jinsi ya kufanya ili uweze kuwa mtu mzuri katika jamii, badala ya kuogopwa au kuonekana hufai katika jamii.

5. Kila mtu na maisha yake...!

Mara nyingi roho mbaya huletwa na chuki binafsi na choyo cha mtu. Mtu anasahau kuwa kila mtu na maisha yake na mtoaji ni Mungu mwenyezi. Usifikirie hata siku moja kuwa unaweza kuzuia riziki ya mtu, Hata siku moja.

Mawasiliano kadidi2@yahoo.com

No comments: