Saturday, April 24, 2010

Umeisikia hii !!!
Hii imetokea huko kwa majirani zetu unaweza usiamini ila ndio imetokea, Twende kazi kama kawaida jana asubuhi kama kawaida yangu nilikuwa nasikiliza kipindi flani kupitia redio moja tena maarufu hapa jijini.
Nikakutana na kisange hiki nacho ni juu ya vituo vyote vya redio kupewa siku kumi na moja kujianda na utaratibu mpya wa kuweka sauti za wanyama na milio ya mitutu badala ya miziki na hii ni kwa ajili ya kurejesha maadili .
Naatakae kaidi atakiona huko ni amri tu ila nikaweza kusikiliza maoni ya watu wanchi hiyo ya somalia wakisema serikari yao inafuatilia mambo ambayo hayana msingi na kuacha yale ya umuhimu . nyie mnasemaje wakublog wenzangu.

No comments: