Thursday, April 29, 2010

Mvua Zinazoendelea kunyesha maeneo

mbalimbali Jijini Dar es Salaam!!!

Hii ni barabara ya Nyerere Road Banda la ngozi,hali si shwari

maeneo hayo kwani barabara imefunikwa na maji haionekani

hata kidogo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini.

Hii ndio hali halisi ya barabara ya Nyerere Road kuelekea Airport

,mvua hizi husababisha baadhi bya magari kuzimika katikati ya

barabara kutokana na wingi wa maji...Lakini nani wakulaumiwa

kama sio TANROADS kuwa na miundo mbinu mibovu wakati

barabara hizi zinapojengwa?

Kwa wale wenye vigari vya chini kuna hati hati ya magari

yenu kuzimika katikati ya barabara kutokana na mimaji

inayojaa kwenye barabara ya Nyerere kuelekea Airport.

Kati ya Mvua na Jua Bora nini?kwa

hali hii nafikiri

hapa jibu utapata kwa jay mo na wimbo mvua

na jua bora nini .

No comments: