Wednesday, April 21, 2010

Maharamia wa kisomali wameteka boti tatu za kuvua samaki za Thailand katika bahari ya Hindi.
Jeshi la wanamaji wa Umoja wa Ulaya limelielezea shambulio hilo kuwa la mwanzo kufanyika mbali sana na pwani ya Somalia.

Msemaji wa jeshi la Umoja wa Ulaya amesema boti hizo tatu, zilizobeba jumla ya mabaharia 77, zilitekwa siku ya Jumapili.

Amesema shambulio hilo limefanyika mbali na eneo ambalo jeshi hilo linafanyia shughuli zake, takriban kilomita 2,222 kutoka pwani ya Somalia.

Inasemekana maharamia hao walikuwa wanapeleka boti hizo nchini Somalia.
Mabaharia wote waliopo kwenye boti hizo, MV Prantalay 11, 12 na 14 zinaripotiwa kumilikiwa na Thailand.

No comments: