Thursday, April 29, 2010

Leo nilipata mgeni wa ghafla ofisini kwangu aliyejitambulisha kwa jina la Nabii Titto.Nabii Titto yeye anahubiri matumizi ya pombe kwa kutumia Biblia,anasema kuwa mungu ameruhusu watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi kwa magonjwa mbalimbali .Alikuja ofisini kwangu ili nimsaidie kurekodi kanda na cd mbalimbali zitakazomafanya watu mbalimbali duniani kupata neno lake na kunisihi sana na kuniambia nikubali kwani ilo ndio ombi mungu alilomtuma kwangu.Mimi sikumkubalia ombi lake kwani ninavyoamini mimi na imani yangu ni vitu viwili tofauti.Je Wadau mnasemaje kuhusu Nabii Titto


Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba sahii tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara,Sikuamini maneno yake akatumwa mtu alete pombe na Nabii Titto bila hiyana kudhihirisha umma akakata safari beer,Wadau mpooo


Kipeperushi hiki cha Nabii Titto kiliniacha hoi

Na mtu huyu anadai kuwa yuko mbioni kuanzisha kanisa

Juma Chikoka (Chopa mchopanga) akiwa na Jackline Wolper na Johari wakimsikiliza Nabii Titto kwa umakini mkubwa
haya utayakuta kwa dada j dee.

1 comment:

Anonymous said...

kweli wajinga wengi duniani.watu wanafungua klabu za pombe.viwanda mabaa . sasa huyu mwenda wazimu umempa cheo .unaonekana nawewe ni mfuasi nakuomba muondoe usimpigie debe mshauri aombe tiba.