Monday, April 19, 2010

LUNYASI OYE!
Mwenyekiti wa Simba Mzee Hassan Dalali akilia kwa furaha
Nahodha wa Simba, Nico Nyagawa akipokea Kombe la Ubingwa wa Ligi kuu ya Vodaconeshno jipya jijini Dar jana kutoka kwa mgeni rasmi, Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana Profesa Kapuya ambaye hafichagi kuwa yeye ni Simba damu.
Kocha Msaidizi wa Simba, Amri Saidi, akibebwa na mashabiki wa timu yake baada ya mchezo kumalizika. Amiri Saidi ndiye aliyeshika mikoba jana kwani kocha mkuu wa simba Phiri yuko kwao Zambia akiuguza
Beki wa kushoto wa Yanga, Amiri Maftah akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Simba, Nico Nyagawa.
Wachezaji wa Yanga wakiwasalimia mashabiki wao kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya Vodacom dhidi ya Simba. Hilary Echessa, akishangilia bao la nne aliloifungia timu yake ya Simba wakati wa mchezo wa Ligi ya Vodacom dhidi ya Yanga uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kulia ni Emmanuel Okwi. Simba ilishinda 4-3.
Mchezaji wa Simba, Uhuri Selemani (kulia) akibadilishana jezi na Abdi kassim wa Yanga

Da kwa kweli jana timu ya wana wamsimbazi walifanya kile walichotakiwa kukifanya na pia watani mtachonga sana kuwa mlicheza sana . Ila kama mjuavyo kuwa raha ya gemu si bao jamani na sie tulipata bao nne kwa hiyo msimu huu sisi mkubali ni jogoo tu .

No comments: