Thursday, July 29, 2010

uchaguzi viti maalum mkoa wa dar
Mgeni rasmi ambaye ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar es salaam,Mh Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mh. Sophia Simba.
Mmoja wa washindi waliochaguliwa,Bi. Ritah Mlaki akishangilia mara baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa washindi watano katika Matukio mbalimbali yaliyofanyika jana jijini kwenye uchaguzi wa Wagombea kupitia UWT kwenye mkutano Mkuu Maalum Wa uchaguzi Mkoa wa Dar es salaam uliofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika viwanja vya Sabasaba.
Katika uchaguzi huo wajumbe wa UWT waliwachagua wawakilishi wa makundi mbalimbali kwa ajili ya VITI MAALUUM, Mwenyekiti wa UWT Mkaoni Dar es salaam Zarina Shamte Madabida alikuwa mshindi wa kwanza. na kufuatiwa na Ritah Mlaki, Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mlezi wa Chama mkoa wa DSM Abdulrahman Kinana, na kuhudhuriwa na MWenyekiti wa UWT Taifa Sophia Simba.
Mgombea wa Viti Maalum Janeth Masaburi akiomba kura kwa wanachama.
Wanachama wakigawiwa karatasi kwa ajili ya kupiga kura.

(picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

No comments: