BREKING  NYUUUUUZZZZZ: CHADEMA YAMTANGAZA RASMI DK. SLAA MGOMBEA WAKE WA URAIS  LEO
                                     MWENYEKITI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA  NA MAENDELEO (CHADEMA) MH. FREEMAN MBOWE LEO AMETANGAZA RASMI KWAMBA  CHAMA HICHO KITAMSIMAMISHA KATIBU MKUU WAKE DK. WILBROAD SLAA KUGOMBEA  KITI CHA URAIS KWENYE UCHAGUZI MKUU MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.
MH. MBOWE AMESEMA MCHANA HUU KWENYE  MAKAO MAKUU YA CHADEMA YALIYOKO KINDONDONI JIJINI DAR KWAMBA KWA KAULI  MOJA KAMATI KUU YA CHADEMA ILIYOMALIZA VIKAO VYAKE JANA IMEKUBALIANA KWA  KAULI MOJA KUMUOMBA DK. SLAA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS, NA KWAMBA NAYE  AMEKUBALI.
MBOWE  AMEPANGUA HOJA KIBAO ZILIZOKUWA ZIKIPIGIA UKOPE UAMUZI WA CGHADEMA  KUMPA DK. SLAA NAFASI HIYO AMBAYO MOJA KWA MOJA ATAKUWA HATETEI TENA  KITI CHAKE CHA UBUNGE CHA KARATU, NA KWAMBA ENDAPO ATAKOSA URAIS ATAKUWA  KAMALIZIKA KISIASA.
"OCTOBA 31 DK. SLAA ATAKUWA RAIS WA  NCHI HII SASA UNAPOSEMA ATAKUWA AMEJIMALIZA KISIASA UNA MAANA GANI AMA  NDIO UNAJIMU WENU AMBAO MMESHAUANZA.
"DK.  SLAA NI MTU MAKINI NA MWENYE SIFA ZOTE ZA SIO TU KUWA RAIS BALI PIA  KULETA MABADILIKO MAKUBWA AMBAYO NCHI HII INAYAHITAJI LAKINI HAKUNA WA  KUTEKELEZA", ALISEMA MH. MBOWE KWA KUJIAMINI HUKU AKISHANGILIWA NA  BAADHI YA WANACHAMA WALIOHUDHRIA MKUTANO HUO NA WANAHABARI.
MWENYEKITI  HUYO WA CHADEMA PIA AMEKANUSHA VIKALI UVUMI KWAMBA DK. SLAA AMETUMWA NA  KANISA LA DINI FULANI KUGOMBEA HUO URAIS, NA KUDAI HUO NI UMBEA WA  BAADHI YA MAGAZETI AMBAYO KADAI AIDHA WAANDISHI AMA WAMILIKI WANATUMIKA  KUKIPAKA MATOPE CHADEMA.
"kUNA  VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINABAKA WANANCHI KWA KUANDIKA HABARI ZA  UMBEA NA KUPOTOSHA KWA MANUFAA YAO (WAANDISHI BINAFSI) AMA WAMILIKI WA  VYOMBO HIVYO.
"NAOMBA  BAADHI YA WAANDISHI WENYE TABIA HIYO WAIACHE WASIJE WAKAIPELEKA NCHI  PABAYA", ALISEMA MH. MBOWE HUKU MEZA KUU WALIYOKETI VIONGOZI WAANDAMIZI  WA CHADEMA AKIWEMO NAIBU KATIBU MKUU MH. ZITTO KABWE, WAKITIKISA VICHWA  KUUNGANA NA KAULI ZAKE.
KUHUSU  UBUNGE JIMBO LA KARATU ATALOACHA WAZI DK. SLAA MWENYEKITI WA CHADEMA  KASEMA WAO HAWANA WASIWASI KWANI HAKUNA CHAMA CHENYE YBAVU WA KUTWAA  KITI KATIKA JIMBO HILO AMBALO ALIONGEZEA KWAMBA HALMASHAURI YAKE YA  WILAYA IMEKUWA IKONGOZWA NA CHADEMA KWA MIAKA 10 SASA.
"DK  SLAA PAMOJA NA KUWA CHACHU KUBWA YA USHINDI WA CHADEMA KARATU LAKINI SI  YEYE PEKEE MWENYE UMUHIMU MKUBWA KULE JIMBONI. KUNA VIONGOZI WENZIE NA  WANANCHI AMBAO KWA PAMOJA NDIO WALIOIFANYA CHADEMA ISIMAME.
"HIVYO  KAA UKIHJUA TAYARI KUNA MGOMBEA MAKINI AMESHAANDALIWA NA ATAFANYA  MAKUBWA KAMA ALIYOFANYA DK. SLAA", ALIFAFANUA.
No comments:
Post a Comment