Monday, June 8, 2009

samaki bwawa la mindu waadimika
Baadhi ya wajasiliamali wadogo wakigombea kununua samaki kutoka kwa wavuvi wa Bwawa la Mindu, lililipo Manispaa ya Morogoro wakiwa wamejitosa majini ili kuwawahi kabla ya kufikishwa nchi kavu, hali hiyo inatokana na uhaba wa upatikanaji wa samaki kwa kipindi hiki kutokana na mwanga wa mwezi nyakati za usiku. Baadhi yao wanatoka maneo ya nje ya Manispaa hiyo ikiwemo Tarafa ya Mlali, iliyopo zadi kilometa 25 kutoka mjini Morogoro.
Vijana hawa wanatunga samaki wadogo kwenye kamba baada ya kuvuliwa kutoka Bwawa la Mindu la Mjini hapa, jana tayari kwa kwenda kuwauza sokoni. Hivi sasa samaki katika Bwawa hilo ni adimu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kipindi cha mwana wa mwezi. Picha na mdau wa mji kasoro bahari, John Nditi.

No comments: