Makala ya  Leo..
 MWALIMU NYERERE NATAMANI  UONE 
 TUNAVYOKUENZI....
 MWALIMU Julius Nyerere Baba wa Taifa letu, tumeadhimisha miaka  tisa tangu ulipotutoka Oktoba 14,1999, na tukakupumzisha kwa amani katika Kijiji  ulichozaliwa cha Mwitongo-Butiama mkoani Mara.Tunaendelea kukuenzi baba japo kwa mitindo mbalimbali.Tukikuita baba kwa sababu wewe ni mwasisi wa taifa letu la Tanzania.Baba,ulikuwa Mwalimu wetu na hata leo hii unaendelea kutufundisha katika yale yote uliyotuusia.
Kuondoka kwako kulituachia majonzi mazito ambayo uzito wake haujapungua hadi leo.
Tunazidi kukukumbuka baba na tunaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi yetu ya kukuenzi milele na milele.Baba katika wingi wetu wapo wanaokuenzi au tupo tunaokuenzi kikweli kweli na wapo wanaokuenzi kinakfi.
Kwa sababu hiyo na kwa mara nyingine tunakusii uchungulie duniani na ujisomee na kujionea mwenyewe yale yanayojiri katika harakati za kukuenzi siku hadi siku.
Baba, si unakumbuka kile chama ulichokiasisi mwenyewe,mapema  mwaka huu kilikuenzi wazi wazi pale kilipoamua kufanya kikao chake cha  Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) katika kijiji ulichozaliwa Butiama ambako mwili  wako ilipopumzishwa ukingojea parapanda ya mwisho.kwa mengi zaidi juu ya makala  hii iliyaondaliwa na Hapiness Katabazi bofya na Endelea....>>>>>>>
 
No comments:
Post a Comment