Sunday, August 30, 2009

Haya haya Kuelekea 2010

Wadau watumiaji wa barabara yetu ya mabibo hadi kigogo muda mfupi kabla ya uchaguzi wanaweza wakaanza kupata matunda ya barabara mzuri ila tuombe Mola mambo yaende kasi kama sasa yanavyokwenda maana simnajua tena barabara ikiwa ya lami mambo huwa bam bam hatuvunji magari na tunatumia muda mfupi barabarani na pia itapunguza kidogo foleni zetu za kati kati ya jiji.
Hongereni mamlaka husika kwa kusikia kilio chetu wakazi wa mabibo nyuma ya soko.
Ni mimi mdau ,Mpenda maendeleo.