Tuesday, January 24, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AANZA ZIARA YA MKOA WA TANGA LEO, AKAGUA UKUTA WA KUZUIA MAJI YA BAHARI PANGANI

Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jengo la Ofisi ya Idara ya Maji, lililopo Wilaya ya Pangani, wakati alipoanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo, Januari 24, 2012. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa (kushoto) ni Mkurugenzi wa Maji wa wilaya hiyo, Mohamed Hamis. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ukuta huo unaozuia maji ya Bahari unaobomoka kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi na kutishia amani ya wakazi wa maeneo hayo. Pangani Kivukoni. Picha na Muhidin Sufiani-OMR Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Pangani wakati akitoka kukagua ukuta wa kuzuia maji ya Bahari unaobomoka Pangani Kivukoni. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia ukuta unaozuia maji ya Bahari eneo la Pangani Kivukoni, unaozidi kubomoka kutokana na kujengwa miaka 100 iliyopita na kutishia amani kwa wakazi wa maeneo hayo. Makamu wa Rais ameanza ziara yake ya Mkoa wa Tanga leo Januari 24, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Saturday, January 21, 2012

kipindi cha kijamii cha weekend specila cha wapo redio fm chatimiza miaka 5

Baada ya shughuli nzima ya maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special,kinachorusha na redio ya Wapo FM,wageni waalikwa walipata picha ya pamoja kama ukumbusho muhimu kwao,nje ya jengo la mikutano la Taasisi ya Maendeleo ya Vijana (UVIKIUTA),iliopo Chamazi-Mbagala jijini Dar.

Keki tuliii safi kabisa.

Mmoja wa wageni kutoka meza kuu,Wakili wa Kujitegemea Bw. Emanuel Makene akikata keki kwa ajili ya kulishwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya kipindi hicho ambacho kimekuwa kikipendwa na kusikilizwa sana wanajamii.

Mtangazaji wa Wapo FM,Dada Benedict Mrema akichombeza hapa na pale,huku muasisi wa kipindi cha Weekend Special,Antony Joseph akitaka kuwalisha wageni waalikwa keki iliondaliwa maalum kwa maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi hicho tangu kuanzishwa kwake.

Keki ikigaiwa kwa wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo.

Mmoja wa wasanii kutoka Taasisi ya Maendele ya Vijana (UVIKIUTA) akiwaburudisha wageni waalikwa

Mmoja wa vijana wajasiliamali akifafanua kuhusiana na matatizo mbalimbali wanavyokumbana nayo katika shughuli zao mbalimbali za kila siku za ujasiliamali.

Mtangazaji wa Wapo FM redip,Dada Ritha Chaula akisoma hotuba fupi kuhusiana na maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special,mbele ya meza kuu na wageni waalikwa mbalimbali waliofika.kipindi hicho hurushwa kila siku ya jumamosi kuanzia saa 8 mchana mpaka 11.30 jioni kikiwa na lengo la kuelimisha,na kuipasha jamii maovu yanayotendeka,namna ya kukabiliana nayo na kuyaepuka,sambamba na hayo kipindi hicho pia huibua na kutangaza matukio ya unyanyapaa,unyanyasaji wa kijinsia,ubakaji na ulawiti,kuwapa vijana elimu ya stadi ya maisha ili waweze kujitambu,kujiamini na kujiajiri katika kuyakabili maisha kiuchumi,kuibua migogoro ya ndoa,kupata elimu ya namna ya kutatua na kupata suluhisho la kudumu.



Wadau wakifautilia kongamano wakati likiendelea.
Baadhi ya Watangazaji wa Wapo Fm redio wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijiri ndani ya ukumbi,wakati kongamano la vijana likiendelea.Sho ni DadaRitha Chiwalo,Benedict Mrema na mdau wa Wapo FM.

Pichani kulia ni Dada Faines Mwakatobe kutoka Chuo Kikuu Huria cha jijini Dar akiwatafsiria baadhi ya Walemavu wa kutosikia,ambao pia wameshiriki katika Maadhimisho ya miaka mitano (5) ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na redio Wapo FM, kila siku ya jumamosi.Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kongamano la vijana ambalo lilijadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika nyanja mbalimbali kama vile uchumi,ajira,elimu na mambo mengineyo.

Baadhi ya wadau wa kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM ambao pia wameshiriki katika Maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na redio Wapo FM cha jijini Dar, kila siku ya jumamosi.

Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia kwa makini mijadala iliyokuwa ikitolewa kwenye maadhimisho hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.

Waimbaji wa muziki wa nyimbo za Injili kutoka kundi la Double E likitumbuiza katika maadhimisho hayo.

Mtangazaji wa kipindi cha Wikend Special kinachorushwa na redio ya Wapo FM, ambacho leo kinaadhimisha miaka 5 tangu kuanzishwa kwake, Bw. Antony (kulia), akiwatambulisha viongozi wa vikundi mbalimbali mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani) waliofika kwenye maadhimisho hayo yaliyofanyika leo kwenye viunga vya UVIKIUTA-Chamazi jijini.

Mwakilishi kutoka TYC, Bw. Nyakia Ally akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa (ambao kwa asilimia kubwa ni vijana kutoka sehemu mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Special Wikend kinachorushwa na redio ya Wapo FM, anayefuata ni Wakili wa Kujitegemea Bw. Emanuel Makene, Dr. Nassoro Ally Matuzya kutoka hospitali ya Mwanyanyamala, Mmoja wa wakilishi kutoka chuo kikuu UDSM, Bw. Edward Daniel na shoto ni Mwendesha kipindi cha Wikend Special Bw.Antony Joseph.

Kongamano likiendelea kwa umakini kabisa.

Mmoja wa wanaharakati vijana,Dr Nassoro Ally Matuzya kutoka hospitali ya Mwanyanyamala akifafanua jambo ikiwa ni sehemu ya kongamano la vijana la kuelimishana kuhusiana na mambo mbalimbali zikiwemo changamoto wanazokabiliana/kumbana nazo katika mfumo mzima wa maisha yao ya kila siku.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Pius Senyagwa sambamba na wasanii wengine wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa kwenye maadhimisho hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.

Makofi ya hapa na pale yalikuwepo kutoka kwa wageni waalikwa.

Baadhi ya vijana walioko kwenye Taasisi ya Maendeleo ya Vijana (UVIKIUTA),kutoka Mataifa mbalimbali wakifuatilia mijadala mbalimbali iliokuwa ikizungumzwa kwenye kongamano lililoendana sambamba na maadhimisho ya miaka 5 ya kipindi cha Weekend Special kinachorushwa na redio ya Wapo FM,jijini Dar,maadhimisho hayo yamefanyika kwenye viunga vya taasisi hiyo huko Chamazi-Mbagala jijini Dar.

WATEJA WA M-PESA WENYE AKAUNTI CRDB SASA KUWEKA NA KUTOA FEDHA KUPITIA SIMU YA MKONONI.




Wateja wa Vodacom M-PESA wenye akaunti katika benki ya CRDB sasa wanauwezo wa kuweka na kutoa fedha kutoka katika akaunti zao kupitia simu ya mkononi ya Vodacom iliyosajiliwa na huduma ya M-PESA.

Kuzinduliwa kwa huduma hiyo sasa kunawapa urahisi zaidi wateja wa Vodacom M-PESA kuweka na kuchukua fedha zao kutoka akaunti ya benki kwa urahisi na unafuu zaidi mahali popote nchini na kwa wakati wowote pasi na kulazimika kufika katika tawi la benki ya CRDB..

Huduma hii ya ushirikiano kati ya Benki ya CRDB na kampuni ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-PESA ni ya kwanza nchini na inalenga kuwaondolea usumbufu wateja wa M-PESA wa kupanga foleni ama kutembea umbali mrefu kufuata tawi la Benki.

“Tunapoitambulisha huduma hii mpya inaamaanisha kwamba tumeongeza thamani nyengine katika simu ya mkononi na huduma ya Vodacom M-PESA.Mteja wa M-PESA kuweza kutoa na kuchukua fedha kutoka akaunti zao za CRDB kupitia simu zao za mkononi ni hatua nyengine muhimu ya kujivunia kuwa mteja wa Vodacom”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza.

Huduma ya Vodacom M-PESA ya kwanza sokoni kutoka Vodacom mtandando unaoongoza nchini ni kielelezo makini cha ubunifu na namna ambavyo Vodacom imedhamiria kubadili maisha ya watu kupitia teknolojia ya simu za mkononi.

Ikiwa na mawakala zaidi 20,000 nchi nzima M-PESA inabakia kuwa huduma salama zaidi, ya haraka, uhakika na yenye kuaminika kwa ajli ya kuweka na kutuma fedha, kufanya malipo ya huduma na manunuzi mbalimbali, kulipia kodi, kuchangia pensheni pamoja na kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya sabini na tano ulimwenguni.

“Hakuna mteja wa Vodacom M-pesa atakaesimama kwenye foleni au kulazimika kutembea umbali mrefu kufuata tawi la benki yake ya CRDB, sasa wataweka na kutoa fedha wakati wowte na mahali popote bila kuathiri shughuli nyengine za kijamii na kimaendeleo ni wazi maisha yamekuwa rahisi zaidi.”Aliongeza Bw. Rene

Tangu ilipoanzishwa mwaka 2007, huduma ya Vodacom M-PESA imeendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuwa huduma yenye usalam zaidi, yenye mtandao mpana wa mawakala mijini na vijijini na hivyo kuchangia maendeleo ya jamii na biashara nchini kwa kuinua vipato vya wananachi kupitia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Kuweka fedha katika akaunti ya CRDB kutoka akaunti ya M-PESA,hatua ni kama ifuatavyo

I. Piga *150#
II. Chagua kulipia bili
III. Ingiza namabri ya biashara ambayo ni 900500
IV. Ingiza nambari ya kumbukumbu ambayo ni namabri ya akaunti ya benki.
V. Weka kiasi cha fedha mteja anachotaka kutoa katika akaunti ya M-PESA kwenda akaunti ya benki
VI. Ingiza nambari ya siri.
VII. Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha muamala.

Baada ya hatua hizi mteja atapokea mara moja ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA kuthibitisha muamala na baada ya dakika 8 atapokea ujumbe kutoka benki ya CRDB.

Kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki ya CRDB kwenda M-PESA hatua ni kama ifuatavyo

I. Piga *150*03#
II. Ingzia nambari ya siri
III. Chagua nambari 3 (Hamisha fedha)
IV. Chagua nambari 3 (M-PESA)
V. Chagua nambari ya akaunti yako ya Benki
VI. Thibitisha nambari yako ya simu
VII. Ingiza kiasi cha fedha unachotaka kuhamisha
VIII. Thibitisha au batilisha. Na baada ya hapo utapokea ujumbe mfupi wa maneno – SMS kutoka M-PESA na pia Benki ya CRDB unaothibitisha zoezi hili.

Ili kuwa na uwezo wa kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda M-PESA ni LAZIMA kwanza mteja wa M-PESA ajisajili CRDB.

Usajili huo hufanyika MARA MOJA TU na kwamba unaweza kufanyika kupitia simu ya mkononi kwa kupiga *150*03# na maelezo ya namna ya kujisajili yatatotekea ambayo mteja atapaswa kuyafuata.

Serikali yasema iko tayari kukutana na madaktari


Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya

Siku chache baada ya Chama cha Madaktari nchini (MAT) kutangaza mgogoro na serikali na kuipa saa 72, serikali imetangaza kuwa ipo tayari kukaa nao meza moja na kuzungumzia masuala ya sekta ya afya.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya, alitoa kauli hiyo jana na kusema kuwa serikali ipo tayari kukaa na MAT kuzungumza kama watakuwa tayari.

Dk. Nkya alisema sakata la madaktari 1,994 waliokuwa katika mazoezi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili waliamua kutoendelea na ratiba zao za mazoezi kwa vitendo baada ya kucheleweshewa posho zao za kila mwezi.

Alisema baada ya kuchelewa kutolewa kwa fedha za posho, wizara ilifanya jitihada ya kuhakikisha fedha hizo zinapatikana haraka.

Alisema serikali ilikuwa ikitoa taarifa katika taasisi walizokuwa wakifanyia kazi kuhusiana na jitihada zinazofanywa ili kutatua tatizo hilo.

“Ieleweke kwamba wataalamu hawa huingia mikataba na hospitali husika na mkataba wanaoingia umeainisha hawatakiwi kugoma au kuanzisha mgomo,” alisema Dk. Nkya.

Dk. Nkya alisema pamoja na wizara kufanya jitihada hizo kuwa suala lao limefanyiwa ufumbuzi, lakini bado walishikilia msimamo wao wa kutorudi vituoni hadi wapokee fedha na kwamba jambo hilo halikuwa la kiungwana.

Alisema baada ya kuona hivyo, wizara ilipeleka wataalamu 51 waliokuwa wakisubiri kuanza mafunzo Januari mwaka huu ili kuchukua nafasi za wataalamu waliokataa kurejea katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuzuia athari ambazo zingeweza kujitokeza kwa wagonjwa. Hata hivyo, alisema katika mgomo huo kuna wenzao 60 ambao hawakugoma.

“Baadhi ya wataalamu waliokuwa wakifanya mazoezi katika vituo kama vya Hospitali ya KCMC, Mount Meru, Bombo, Bugando na Manispaa za Dar es Salaam walitambua jitihada za wizara za kushughulikia tatizo hilo na waliendelea na ratiba yao ya mazoezi kwa vitendo,” alisema.

Alisema waliogoma uongozi wa Muhimbili uliwachukulia hatua na kuwaandikia barua kuwarudisha wizarani na kutaka wapatiwe wataalamu hao.

“Ili kuhakikisha wataalamu hao wanafikia malengo ya mazoezi ya vitendo wizara imeamua kuwapanga katika hospitali mbalimbali ikiwemo Muhimbili, Temeke, Mwananyamala, Aga khan, Amana na Lugalo kwa kuzingatia uwezo wa hospitali,” alisema.

Alisema Januari 16, mwaka huu wataalamu 194 walikuwa wamepewa barua na wameripoti katika vituo walivyopangiwa.

Alisa wizara yake imepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa MAT imewapa saa 72 iwarudishe madakatari hao katika hospitali ya Muhimbili pamoja na kutaka kuondolewa kwa baadhi ya viongozi wa wizara.

Hata hivyo, alisema tamko hilo halijawasilishwa rasmi wizarani na kusisitiza kuwa madakatari hao hawajafukuzwa kufanya mazoezi bali wamepangiwa vituo vingine.

Akizungumzia uamuzi wa MAT kumvua uanachama Mganga Mkuu wa Serikali, Deo Mtasiwa, Dk. Nkya alisema chama hicho hakiwezi kumchukulia hatua bali chombo chenye mamlaka ni Wizara.

Rais wa MAT, Dk. Namala Mkopi, alisema suala hilo watalizungumzia leo na kwamba tamko walilolitoa Jumamosi sio lazime lipelekwe wizarani ndio maana walitoa taarifa kupitia vyombo vya habari.

CHANZO: NIPASHE

Friday, January 20, 2012

AJIRA MPYA ZA WALIMU ZATANGAZWA MAJINA YATOLEWA

Kwanza Tunapenda wasalimu wakubwa wetu Shikamoo na vijana wenzetu Mambo vipi.. Tunatambua kuwa Wanavyuo wenzetu walimu walikuwa hawana kazi kwa muda mrefu Jambo ambalo liliwafanya wengi kuwa na wasi wasi na mwajiri wao. Tunapenda kuwapa tarifa kupitia mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo (www.tzwanavyuo.blogspot.com) kuwa, Walimu wahitimu wote Jana usiku majira ya sa saba Nafasi hizo zilitangazwa Rasmi, Pia sisi Tunapenda kuwasilisha majina ya wanafunzi ambao wamechaguliwa Tunaomba mchukue Muda wenu kutazama kwa umakini majina yenu yote yapo hapa. Hongereni sana.
Imeandaliwa na, Matukio na Wanavyuo Crew

MREMBO AUWAWA NIGERIA KISA FACEBOOK


UHUSIANO wa kimapenzi, ulioanzishwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook, umesababisha kifo cha mrembo nchini Nigeria.

Habari za mtandaoni zinadai kuwa mrembo huyo (jina halikutajwa) pamoja na boyfriend wake (jina pia halijatajwa), walikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu.

Imedaiwa kuwa wakati wawili hao wakiwa kwenye utekelezaji wa hatua za mwanzo za kufunga ndoa, mrembo huyo alimtaarifu boyfriend wake kuwa amepata mpenzi mwingine kwa njia ya Facebook.

Chanzo cha habari kiliiambia tovuti moja ya nchi hiyo kwamba mrembo huyo alianzisha urafiki wa Facebook na kijana mmoja raia wa Marekani (jina halijatajwa) kabla ya kibao kubadilika na kuwa wapenzi.

Chanzo kiliendelea kupasha habari kwamba mrembo huyo na mpenzi wake wa Facebook, walidumisha uhusiano wao kwa njia ya mawasiliano ya simu kwa muda mrefu kabla ya kukata shauri la kuonana ana kwa ana.

“Yule kijana raia wa Marekani alitembelea Nigeria, akafikia hoteli moja kubwa. Yule mrembo akaenda kukutana naye na kutumia muda mrefu chumbani.

“Ni kama baada ya kukutana ndiyo mapenzi yaliongezeka zaidi, kwani alipoondoka hotelini, yule mrembo alirudi kwa boyfriend wake aliyepanga kufunga naye ndoa na kumueleza kwamba mapenzi yamekwisha.


“Baada ya kuambiwa hivyo, kijana aliyekuwa na mategemeo ya kufunga ndoa na mrembo huyo, alimpeleleza mpenzi wake na kubaini mahali ambako kijana kutoka Marekani alifikia.

“Siku iliyofuata alivamia kwenye ile hoteli, akamkuta mpenzi wake na yule kijana wa Facebook, hapo ugomvi mkubwa ulizuka. Ugomvi haukuishia hapo kwa sababu kijana wa Nigeria aliahidi ni lazima aue mtu.

“Siku moja baada ya ugomvi hotelini, kijana wa Nigeria alimteka mpenzi wake na kumuua kwa kumkatakata na silaha inayodhaniwa kuwa ni panga,” alisema mtoa habari huyo.

Kwa mujibu wa mtandao huo mpaka pale habari hiyo inachapishwa, mtuhumiwa wa mauaji alikuwa hajakamatwa.

Iran yataka mazungumzo na Marekani bila masharti

Waokozi wa MV Spice Islander
Umoja wa Falme za Kiarabu umetahadharisha dhidi ya kutokea machafuko zaidi juu ya mgogoro uliopo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku Iran ikitaka majirani zake wa Kiarabu kujitenga na Marekani.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran, Ali Akbar Salehi, amesema amani na uthabiti wa eneo hilo ndio nia ya nchi hiyo lakini akaonya mataifa jirani kutojiweka katika hali ya hatari kwa kujiweka karibu sana na Marekani. Majirani wa nchi za Kiarabu wa Iran ni washirika wakuu wa Marekani wanaosema kwamba hawatakubali hatua yoyote ya kufunga mlango wa bahari ya Hormuz.

Ali Akbar amesema Marekani inapaswa kujitokeza wazi wazi na kusema iwapo ina nia ya kufanya mazungumzo na Tehran, na inapaswa kufanya hivyo bila ya kuwawekea vikwazo vyovyote. Waziri huyo aliyasema haya baada ya kupokea barua kutoka kwa Rais Barack Obama wa Marekani juu ya kufungwa kwa mlango wa hormuz. habari zaidi juu ya barua hiyo bado haijatolewa. Ikulu ya Marekani imekataa pia kutoa maoni juu ya barua hiyo.

Kwa sasa kuna hali ya wasiwasi kati ya Iran na Marekani kuhusu mpango wake wa nuklia, ambapo Marekani na mataifa mengine yenye nguvu duniani wanasema Iran ina nia ya kutengeneza silaha hizo za atomiki jambo ambalo Iran inakanusha Vikali.

Rais Barack Obama wa Marekani.
Rais Barack Obama wa Marekani.
Iran imetishia kufunga mlango wa bahari ya Hormuz ambayo hutumika sana katika kusafirisha mafuta, iwapo mataifa ya Ulaya yatasisitiza nchi hiyo kuwekewa vikwazo katika biashara zake na pia kuzuiliwa kwa mali zake katika benki kuu nchini humo. Iwapo Iran itatekeleza onyo hilo la kuufunga mlango wa bahari ya Hormuz basi kunaweza kutokea mgogoro mkubwa katika jamii ya Mashariki ya Kati.

Hata hiyo, mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu kukubaliana juu ya ya vikwazo dhidi ya Tehran. Iwapo vikwazo vipya vya Marekani vilivyowekwa saini na rais wa nchi hiyo Barrack Obama siku ya mkesha wa mwaka mpya vitapitishwa, haitaruhusu mataifa mengine kulipia mafuta ya Iran.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nguvu za Atomiki amesema ni jukumu lake kueleza dunia kuhusu uwezekano wa hatua za kijeshi juu ya mpango wa nuklia wa Iran akiweka msisimko mkubwa kabla ya mkutano wa wanachama wa shirika hilo utakaofanyika Januari 29 hadi 31. Nalo shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kitu wanachokijua kwa sasa ni kuwepo kwa harakati za kutengeneza silaha za nyuklia na kwa sasa wanataka kufanya kila juhudi kujua undani wa habari hiyo.

Tuesday, January 17, 2012

Ni safari ya Regia Mtema

Maafisa Usalama wa Bunge (Sargent at arms) wakiwa wamebeba Sanduku lililohifadhi mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA kutoka Kilombero mkoani Morogoro, Marehemu Regia Mtema aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajali. Mwili huu ulikuwa unatolewa katika Hospitali ya taifa Muhimbili mapema leo kwenda Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo kunashughuli ya kuuaga mwili wa Marehemu kitaifa na baade kusafirishwa hadi Ifakara kwa Maziko yatakayo fanyika kesho.

Maafisa Usalama wa Bunge (Sargent at arms) wakiweka jeneza lenye mwili wa marehemu Mh Regia Mtema MB kwenye gari tayari kuelekea karimjee kwa heshima za mwisho asubuhi hii.


Friday, January 6, 2012

Majambazi wavamia ndege ya dhahabu


Pichani: Wakazi wa Wilaya ya Geita mkoani Mwanza, wakiangalia mwili wa mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi (jina hajafahamika), akiwa ni mmoja wa watu wanne waliyovamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), akiwa amekufa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika jaribio hilo la kutka kupora dhahabu jana. (Picha na Sitta Tumma)
WATU wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM), na kuteka ndege ya kubeba madini hayo na kupora vitofali 68 vya dhahabu iliyokuwa ikisafirishwa kutoka mgodi huo kwenda nje ya nchi yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 130.

Hata hivyo, majambazi hao walishindwa kuondoka na dhahabu hiyo baada ya polisi wilayani hapa kuwahi kufika eneo la tukio na kuiokoa, baada ya kupambana na majambazi hao kwa
kurushiana risasi na kuua mmoja.

Dhahabu iliyonusurika kuporwa na majambazi hao kwa mujibu wa madai ya mmoja wa polisi aliyeikagua ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, ilikuwa ni zaidi ya kilo 1,000.

Polisi huyo alidai kuwa dhahabu hiyo ilikuwa imegawanywa katika makasha 16 huku kila kasha likiwa na vitofali vinne vya dhahabu na kila kitofali kikiwa na uzito wa kilo 25.

Hata hivyo, Ofisa Madini mkazi wa Kanda ya Geita, Juma Sementa, ambaye ofisi yake imekuwa ikikagua na kuhakiki dhahabu kabla ya kusafirishwa kila wiki na mgodi huo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu uzito kamili wa dhahabu iliyokaguliwa na ofisi yake juzi kabla ya kusafirishwa
jana, alitofautiana na madai ya polisi.

Sementa alisema ofisi yake ilikagua makasha 25 na kila kasha likiwa na kitofali kimoja cha dhahabu chenye uzito wa kati ya kilo tano na 30.

Katika tukio hilo la aina yake, polisi walimuua mtuhumiwa mmoja baada ya kummiminia risasi kifuani, ingawa tayari alikuwa amejeruhiwa na mmoja wa walinzi wa mgodi huo ambaye ni
raia wa Afrika Kusini.

Tukio hilo lilitokea jana saa 5.55 adhuhuri katika uwanja wa ndege wa mgodi huo ulioko umbali wa kilometa tano kutoka katikati ya mji wa Geita.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa polisi wilayani hapa, uchunguzi wa awali ulionesha kuwa majambazi wapatao
wanne walivamia mgodi huo wakiingilia lango kuu la uwanja huo wa ndege.

Ilielezwa kuwa majambazi hao wakiwa na mabomu ya kutupa kwa mkono, bunduki aina ya SMG na bastola, waliishambulia kwa risasi ndege iliyokuwa ikipakia dhahabu kutoka kwenye gari maalumu.

“Hali hiyo iliwafanya walinzi wa mgodi huo waliokuwa wakilinda usalama wa mali iliyokuwa ikisafirishwa, kutimua mbio, lakini alibaki Mzungu raia wa Afrika Kusini mfanyakazi wa
mgodi huo, aliyekuwa na bastola.

“Raia huyo wa Afrika Kusini alipambana na majambazi hao kwa kuwafyatulia risasi,’’ alisema mmoja wa maofisa wa Polisi katika mahojiano maalumu na gazeti hili.

Ilidaiwa kuwa wakati raia huyo akiendelea kufyatuliana risasi na mmoja wa majambazi hao, aliishiwa risasi na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye mkono na kukimbia kuokoa maisha
yake.

Hata hivyo, baada ya muda mfupi, inadaiwa askari Polisi walifika na kupambana na majambazi hao ambapo watatu walitimua mbio na kubaki mmoja ambaye tayari alikuwa amejeruhiwa
na Mzungu huyo; akashambuliana kwa risasi na polisi, lakini alizidiwa na kuuawa.

Bastola, mabomu, bunduki
Jambazi aliyeuawa bado hajatambuliwa jina na alikutwa na bastola aina ya Chenese namba 0048467 ikiwa na risasi sita, na bunduki aina ya SMG namba UA89381997 inayoonekana kusajiliwa Uganda.

Pia alikutwa na mabomu manne ya kutupa kwa mkono, magazini nne na risasi 60 ambazo hazijatumika, huku akiwa amevalia nguo za kawaida nguo nne ndani na ya juu ikiwa ni sare za
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jambazi huyo naye alimjeruhi kwa risasi mfanyakazi mwingine wa mgodi huo, raia wa Afrika Kusini aliyetambuliwa kwa jina la Engenas Van Der Schuffs, baada ya kumpiga risasi kwenye mkono wa kulia.

Marubani wa ndege iliyoshambuliwa yenye namba SH-TZX walitambuliwa kwa majina ya Meja Kondo Hamza na Hamdan Salehe.

Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio zilisema ndege hiyo ilishindwa kuondoka kwenye uwanja huo kutokana na moja ya mabawa yake kutobolewa kwa risasi.
Chanzo:Habari Leo
Tiger Woods’ ex-wife bulldozes $12 million home

Courtesy of Pacific Coast News

There are times when divorce forces people to do strange things. Burn sheets. Throw out clothes. Toss rings into the ocean. But when you get $100 million in your divorce, you can trump just about anything and that's what happened with Tiger Woods' ex-wife when she bought a $12 million home and bulldozed the whole thing.

[Check the before picture above and the after picture after the jump]

Yes, according to TMZ, Elin Nordegren bought a $12 million home in North Palm Beach, Fla., but didn't like it, and has plowed the whole thing.

The house, which had six bedrooms and eight bathrooms, is now just rubble, with no word yet on what is going to replace the beautiful building you see above, but I guess when you have nine figures in the bank, it doesn't really matter what you want.

I guess we can all applaud Elin on not rolling over after all this happened and continuing on with her life. But I think we can all agree on one thing: Why in the world is she still in Florida? Wouldn't you want to move back home for good?