Tuesday, March 16, 2010

Kero Hii: Wamachinga Wa Manzese!
Kaka Kadidi pole sana na kazi ya kutupa habari za moto moto.

Habari niliyonayo ni kero lakini sina uhakika kama ina nafasi katika blogu yako.
Kero yenyewe ni ndugu zetu wanaofanya biashara barabarani katika barabara ya morogoro road kwenye kituo cha mabasi cha manzese cha kutokea mjini. Kwa kweli wanakela sana wanafanya barabara iwe nyembamba na kuleta foleni ya magari.

Mheshimiwa Lukuvi, Kova na vijana wako na Mzee Kimbisa bila kumsahau kaka Jordan naomba mlitupie macho hili linakera.

Wenu

Muganyizi Kilibata

No comments: