Wednesday, March 18, 2009

mama kikwete aasa wanaume wa kikurya dhidi ya kupiga mai waifu wao
Mama salma kikwete
Na Anna Nkinda wa Maelezo


Mama Salma Kikwete amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.

Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.

“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sana sasa sijui kama ni kweli au la, lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli ”, alisema.
"Tatizo langu mie kwa watani zangu hawa ni hapo, je kinamama si wataona waume zao hawawapendi?
"Nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya huanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba, kweli hayo watani???", alihoji.
Mama Kikwete pia aliwataka wakazi hao kuachana na imani za kishirikina za kuamini kuwa ukiwaua walemavu wa ngozi (albino) utapata utajiri na kuwataka kuwafichua wauaji wa albino.
“Kila mtu ana haki ya kuishi kama mwingine si vyema kuwafanya albino hawana haki ya kuishi na kuwaua pasipo sababu”.
“Acheni kuua albino kwani utajiri hauji kwa kuuza viungo vyao bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kijituma kwa kufanya hivyo mtafanikiwa na kuondokana na umaskini”, alisema.

No comments: