Inawezekana !!!!!

Jiamini unaweza na ufanye unachoamini!!

Thursday, December 30, 2010

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. ANNE SEMBAMBA MAKINDA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Sembamba Makinda akishuka kwenye gari lake kuelekea ofisi za Bunge mjini Dodoma.

SPIKA mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Semamba Makinda, (61) ambaye alichaguliwa hivi karibuni amefanikiwa kufanya mahojiano maalum na mtandao wa MO BLOG ya Jijini Dar es Salaam, na katika mahoajiano hayo aligusia vipengele vifuatavyo:

-Asema hataki kuondoka kwa shangwe za aibu

-Asisitiza muda wa miaka 40 Bungeni inatosha

-Aahidi kuhimili mikikimikiki ya wabunge vijana

Kupata mahojiano haya kwa kina bonyeza hapa:

http://www.mohammeddewji.com/blog/?cat=5
Posted by Safari at Thursday, December 30, 2010 1 comment:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Wednesday, December 29, 2010

Tangazo !!
Kwa yule anaehitaji nyumba maeneo ya sinza
awasiliane nami kwa namba 0754023353
Posted by Safari at Wednesday, December 29, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
BREAKING NYUUUZZZZ:
CHENGE AFANIKIWA KUKWEPA LUPANGO
KWAKUTOA FAINI YA LAKI 7 LEO
Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali za juu katika serikali ya Tanzania ikiwamo ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, leo alipona kutupwa jela miaka mitatu baada ya kulipa faini ya sh 700,000 katika kesi yake kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake wawili.

Hakimu Mfawidhi Kwey Rusema wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo.

Rusema alisema kutokana na ushahidi wa watu sita uliotolewa,mahakamani imemhuona na hatia ya makosa manne ambapo alimuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya sh 700,000.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rusema alisema kuwa,Mahakama imemkuta na katika makosa yote manne na kwa kosa la kwanza na la pili alitakiwa alipe faini ya sh 250,000 kwa kila kosa ambayo ni sawa na sh 500,000 au kwenda jela miaka miwili na katika shitaka la tatu na la nne alitakiwa kulipa faini ya sh 100,000 au kwenda jela mwaka mmoja.

Chenge alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kuendesha gari kwa uzembe na kusababisha vifo vya wanawake waWili,uharibifu wa mali na kuendesha gari bila kuwa na bima.
Posted by Safari at Wednesday, December 29, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Tuesday, December 28, 2010

AU YAMTAKA RAILA KUSULUHISHA MGOGORO WA IVORY COAST…!!!

Bw.Raila Odinga


Umoja wa Afrika AU umemtaka Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga kuongoza juhudi za umoja huo katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa unaofukuta nchini Ivory Coast ambako marais wawili tayari wameapishwa.

Juhudi hizo za kutafuta muafaka nchini Ivory Coast pia zinahusisha wakuu watatu wa mataifa ya Afrika.

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Jean Ping amesema amemuomba Bw. Odinga kufuatilia hali ilivyo nchini humo na kuimarisha juhudi zinazochukuliwa kumaliza machafuko.

Akizungumza na vyombo vya habari, Bw. Odinga ametangaza kukubali jukumu alilopewa na Umoja wa Afrika AU, na kuahidi kuwa katika mgogoro huo hatafungamana na upande wowote ili aweze kuleta amani na maridhiano nchini Ivory Coast.

Aidha Bw. Raila ameongeza kusema kuwa Gbagbo anapaswa kupewa uhakika kuwa hakuna hatua mbaya zitakazochukuliwa dhidi yake kwani naye amekuwa akipigania demokrasi nchini humo.

Posted by Safari at Tuesday, December 28, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

BREAKING NEWS…!!!

Risasi zinarindima katika Maeneo ya Karume njia ya kuelekea Ilala na Buguruni kwa ajili ya kuzuia maandamano ya wanachama wa Chama cha CUF….Mwandishi wetu yuko eneo la tukio habari kamili baadaye.

Posted by Safari at Tuesday, December 28, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

WANANCHI AUSTRALIA WAKIMBIA MAFURIKO KATIKA JIMBO LA QUEENSLAND…!!!

Baadhi ya nyumba zilizokumbwa na mafuriko hayo


Mafuriko makubwa yaliyolikumba eneo la kaskazini –mashariki ya Australia yamewalazimisha maelfu ya wakazi wa maeneo hayo kukimbia huku yakiharibu barabara zaidi ya mia tatu (300).

Mafuriko hayo pia yamesababisha hasara ya mamilioni ya dola katika mashamba ya mazao ya alizeti na pamba.

Kufuatia siku kadhaa za kunyesha mvua mfululizo serikali katika jimbo la Queensland imetangaza maeneo kadhaa kuwa ukanda wa janga.

Hii inakuwa ni desemba ya kwanza kuwa na mvua kubwa na kusababisha mafuriko katika mji mkuu wa jimbo hilo Brisbane kwa kipindi cha zaidi ya miaka 150.

Miji ya ndani ya Theodore, Chinchilla na Dalby imefunikwa na maji, huku mji jirani wa Warra, na miji ya Alpha na Jericho magharibi mwa Emerald, pia imetangazwa kuwa maeneo ya janga

Posted by Safari at Tuesday, December 28, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Bagamoyo panazidi kupendeza.
Boma la Bagamoyo likipigwa sop-sop ili liwe kama mengine kibao yaliyokarabatiwa ama yanayokarabatiwa sasa na kuufanya mji huu mkongwe uwakewake na uzidi kuvutia watalii wa nje na wa ndani
mojawapo ya majengo yaliyokarabatiwa pamoja na barabara ambayo imejengwa kama iliyokuwa enzi hizo, sio kwa lami bali vitofali
Jengo lingine ambalo sasa linawaka ile mbaya baada ya
ukarabati na barabara mpya mbele yake

Hii ndiyo posta ya kwanza Afrika Mashariki karibu na bandari ya Bagamoyo. Hivi sasa inakarabatiwa na kuwa sehemu ya hoteli ya Millenium inayomalizia jengo lake kuu linaloangalia bahari kwa nyuma ya hii posta
Jengo jipya la Millenium bega kwa bega na posta ya zamani
Posted by Safari at Tuesday, December 28, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
MSAADA TUTANI


Naomba utusaidie kuweka picha hizi na ujumbe huu
kwenye Globu ya Jamii. Tunajua zitawafikia wahusika.

Yaani ni aibu kubwa wakazi wa Sinza “ A”, tumeachiwa matakata nyumbani kwetu kwa zaidi ya mwezi mmoja na siku kadhaa sasa. Juzi tu kabla ya krismas wakusanyaji ushuru wa matakata walipita lakini wananchi wamechukia sana sijui kama kuna hata mmoja alijitokeza kulipa.

Mapanya yaliyokufa mawiki kadhaa yaliyopita harufu zilizoko ndani majumbani kwetu inatisha. Krismas tumebakia na mitakataka ndani. Wengine wamezidiwa ndani ya magetini yao na wameweka nje ya geti zao na ni uchafu wa kutisha.

Hii picha imechukuliwa mtaa mmoja tu maeneo ya karibu na blue-bird guest house kuelekea karibu na hospitali ya kwa babu ukitokea Maeda Bara. Ninasema harufu ni ya kutisha na tumekaa nayo karibu kwa mwezi mmoja na siku kadhaa. Alikuwepo mkandarasi mzuri sana ktk siku za hivi karibu aliyekuwa anaitwa KIMANGELE. Lakini sijui nini kilitokea akaletwa mtu ambaye waliona atafanya hiyo kazi, matokeo yake ni hali hii tuliyonayo sasa.

Hivi kweli tunakwenda au tunaelekea wapi? Inamaaana suala kama hili lazima liende Ikulu ndiyo lipatiwe ufumbuzi? Watu wamechukia sana. Wanauliza uongozi uko wapi? Mwenyekiti wa serikali za mtaa hapatikani kabisa maana ameshapigiwa makelele ya kutosha na nadhani kwa usalama wake amezima simu. Sijui kama kweli anapatiwa msaada mara baada ya kuwasilisha maombi au matatizo yetu. Kama tumeshindwa kuzoa hata takataka zetu tu hivi tunakoelekea ni wapi?

Moshi, Arusha na Mwanza wanafanyaje miji yao inakuwa mizuri. Tunaomba taarifa hizi ziwafikie wahusika, na tunaomba ofisi husika ziitishe mkutano na mara nyingi tunakutana pale Meeda Bar na mara hii tunaomba ulinzi wa kutosha maana wananchi wamechukia mno. Huku ni kunyanyasana kabisa. Tunaadhibiwa kwa makusudi.

Nani ambaye hajui takataka zikinyeshewa na mvua zinanuka na kutoka wadudu? Inabidi tuchemshe maji ya moto, kumwaka ili wadudu wanaotoka kwenye matakata wasiingine ndani. Mainzi ni kila kona inabidi upigie Dawa ya MBU kama Xpel au Rungu kila siku ili kuuwa wadudu. Ukisema utoe matakataka getini geti lako litapandwa kwa harufu na watu watakuona wewe ni mchafu wa kupindukia.

Wengine wamefanya hivyo baada ya matakataka kujaa getini. Hivi tunakwenda wapi na hii Sinza yetu? Hivi lazima agizo litoke kwa Waziri Mkuu ili uchafu uzolewe? Ukitaka kujua ukweli mtu yeyote kutoka serikali anayetutakia maisha mazuri, tusipate kipindupindu aje na apite katika nyumba chache tu na ajue jinsi watu walivyoumizwa na hizi takataka. Hata mtu ukiwa msafi namna gani mainzi lazima yawe sehemu ya maisha ya kila siku kwa mlundikano huu wa takataka.

Tunaomba wahusika wafuatilie hili suala la sivyo Sinza italipuka kwa kipindupindu. Hizi picha nimechukua mtaa mmoja tu yaani ni karibu nyumba kama 8 hivi. Inatisha kwa wakazi wa Sinza A. Sijui sinza B, nk. Tunaomba tusaidiwe. Na pia tunaomba kufanyike mkutano mwingine na uongozi wa mkoa ikiwezekana.
Posted by Safari at Tuesday, December 28, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Sunday, December 26, 2010

FFU wa Ngoma Africa Band Kukiwasha nchini Serbia 2011



FFU ! Wa Ngoma Africa band Kuvamia Belgrad,Serbia!

FFU wa Ngoma Africa band kupeleka mzimu wa Dansi nchini Serbia ,January 2011

Bendi maarufu ya mziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU,wanatarijiwa kutumbuiza katika mji wa Belgrad,nchini Serbia,ulaya ya mashariki katika maonyesho ya Film and music festival yatakayoanza tarehe 5 hadi 12 January 2011,
Pia wakazi wa mji wa Montenegro watavamiwa na mziki huo wa dansi kutoka kwa ffu wa Ngoma Africa band yenye maskani yake nchini Ujerumani.
Ni juzi juzi tu wakali hawa wa mziki wa dansi na "MZIMU WA MZIKI" walikuwa wakipeperusha CD maalum "Jakaya Kikwete 2010" .
Toka bendi hiyo ipelekewe mwaliko wa kwenda SERBIA ,wanamziki wa bendi hiyo wamshikwa na matumbo joto! kutokana
historia ya nchi ya SERBIA ambayo miaka ya nyuma ilikuwa na vita....Pia ziara ya wakali hao Ngoma Africa band,ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kwenda Serbia

wasikilize hapa www.myspace.com/thengomaafrica pia www.unheardradio.com/The_Ngoma_Africa_band
Posted by Safari at Sunday, December 26, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Marehem Hassan Jumanne Makunja
Amezaliwa 4-03-1964 amefariki 19-Dec-2010
Marehem Hassan Jumanne Makunja ni mdogo wake Ras makunja.
Late Hassan Makunja amefariki dunia uko Utete,Rufiji,mkoani Pwani
siku ya 19.December 2010 na kuzikwa 20.12.2010.
Marehem Hassan Makunja alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya vidonda vya tumbo,
alikwenda mjini utete,Rufiji kwa mapuziko na kumtembela mama yake mzazi,
Ndipo umauti ukamkuta .
Familia ya marehem inasikitika kuwajulisha jamaa na marafiki taarifa hii ya msiba wa Ndugu Hassan Jumanne Makunja,kuwa hatunaye tena.
Rambi rambi wasiliana namba hii 0787532929 au 0718893419, Bi.Ummy Makunja
Posted by Safari at Sunday, December 26, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
JOKE!!
A three-year-old walked up to a pregnant lady while waiting with his
mother
in the doctors office.
He inquisitively asked the lady, "Why is your stomach so big?"
She replied, "I'm having a baby."
With big eyes, he asked, "Is the baby in your stomach?"
She answered, "He sure is."
Then the little boy, with a puzzled look, asked, "Is it a good baby?"
She said, "Oh, yes. It's a real good baby."
With an even more surprised and shocked look, he asked,
.
.
.
.

Then why did you eat him?"
Posted by Safari at Sunday, December 26, 2010 1 comment:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Balance sheet of life

Our Birth is our Opening Balance

Our Death is our Closing Balance ?

Our Prejudiced Views are our Liabilities

Our Creative Ideas are our Assets

Heart is our Current Asset

Soul is our Fixed Asset

Brain is our Fixed Deposit

Thoughts are our Current Account

Achievements are our Capital

Character & Morals, our Stock-in-Trade

Friends are our General Reserves

Values & Behaviour are our Goodwill

Patience is our Interest Earned

Love is our Dividend

Children are our Bonus Issues

Education is Brands / Patents

Knowledge is our Investment

Experience is our Premium Account



Our aim is, to tally the Balance Sheet accurately.. ..... and the goal is, to get the 'Best Presented Accounts' Award
HAVE A NICE DAY
Posted by Safari at Sunday, December 26, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Tangazo
Kwa wale wanaohitaji Nyumba ya kupanga!!
Kuna nyumba ambayo iko maeneo ya sinza inapangishwa kwa miaka mitano. Hii inamaana kuwa unailipia pesa yote ya miaka mitano na unatlipia miaka mitano hiyo kwa kiasi mtakachokubalina na utaepuka kupanda panda kwa kila mwaka kwa kodi. Kazi kwako na kizuri zaidi ni nyumba mpya tunamalizia kidogo utakapotoa pesa yako na pia utakuwa wa kwanza kuingia kuna parking ya gari moja. Na pia ni ghorofani unajitegemea huko juu bila kukutana na wachini yako.
tuwasiliane kwa namba 0754023353.
Nb. hakuna dalali hapo wasiliana na namba hiyo hapo juu.
Kwa wale wanaohitaji.

Posted by Safari at Sunday, December 26, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Saturday, December 25, 2010

Jeshi la Magereza Sasa Kujiendesha Kisayansi


Waziri wa Mambo ya Ndani,Shamsi Vuai Nahodha(kushoto)akipewa maelezo na maofisa wa Magereza, namna mfumo wa Teknohama katika jeshi hilo unavyofanya kazi.
----
Na Selemani Nzaro
JESHI la Magereza katika Mkoa wa Dar es Salaam limeingia katika mfumo mpya wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Teknohama) katika uhalifu kwa Jeshi la Magereza.

Mfumo huo uliozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita utawezesha maofisa Magereza wakiwa makao makuu kupata taarifa za uhalifu wa wafungwa wakiwa magerezani, ambapo ofisa atafuatilia rekodi zinazoweka pasipo ulazima wa kusafiri.


Mfumo huo wa kisasa kabisa utaliwezesha Jeshi la Magereza kuweka taarifa za wahalifu yaani wafungwa na mahabusu katika mfumo huo hali itakayorahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu katika makao makuu.


Mfumo huo utahusisha wahalifu kutoka katika magereza matatu ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam. Taarifa za wahalifu kutoka katika magereza matatu ndani ya mkoa huo zitapatikana makao makuu ya jeshi hilo yaliyopo katikati ya jiji.


Hii ina maana kama taarifa za mhalifu zimesahaulika askari hatalazimika kusafiri hadi katika gereza husika ili kupata taarifa hizo. Magereza yatakayohusika katika mpango huu ni yale ya Ukonga, Keko na Segerea.


Kukamilika kwa mradi huu wa Teknohama kunahitimisha safari ndefu ya kuuandaa iliyoanza mwaka 2000. Mwaka huo Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ilianzisha mradi uliokwenda kwa jina la ‘Kuimarisha Uwezo ili Kuboresha

Hadhi ya Haki za Binadamu Tanzania’.

Posted by Safari at Saturday, December 25, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Wapenzi wa blog hii ya Inawezekana

Nawatakia xmass njema na mwaka mpya 2011

wenye changamoto kibao.

wenu kadidi2.

Posted by Safari at Saturday, December 25, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
NYOTA WANAOTAMBA BONGO KWA SASA
MARLAW, DIAMON NA ALI KIBA NDIO NYOTA WALIO JUU KATIKA MUZIKI WA KIZAZI CHA LEO YAANI BONGO FLEVA. WOTE WANA VIBAO LUKUKI AMBAVYO VIMESHIKA CHATI KILA VINAPOTOKA NA WOTE WAMESHINDA TUZO MBALIMBALI NA HAWAONESHI KUWA WATACHOKA HIVI KARIBUNI.
Posted by Safari at Saturday, December 25, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima
SHIRIKA la Umeme (Tanesco) jana lilitangaza mgawo mpya na mkubwa wa nishati hiyo ambao utavifanya viwanda, maduka, ofisi na makazi kukosa umeme kwa kati ya masaa sita hadi 12 kwa muda wa mwezi mzima.

Tangazo hilo la mgawo ambalo limekuja katika kipindi ambacho mjadala wa jenereta za kampuni ya Dowans ukiwa umeibuka tena, linatarajiwa kuongeza gharama za maisha kutokana na ukweli kuwa viwanda vingi vitalazimika kutumia jenereta katika uzalishaji licha ya Tanesco kutangaza kuwa vitapewa umeme nyakati za mchana.

Wananchi ambao kipato chao kinategemea biashara ya samaki, saluni, na vinywaji pia wataguswa na makali hayo moja kwa moja wakati mabenki, vituo vya mafuta, mahoteli na makampuni mengine ya kutoa huduma yatajikuta yakiingia gharama kubwa katika utendaji wao.

Tangazo la Tanesco limetolewa wakati kukiwa na ahadi kemkem za kumaliza kabisa tatizo la mgawo wa umeme, huku Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ikiwa imeliruhusu shirika hilo la umma kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 18.5.

"Mgawo huu wa umeme umeshaanza kwenye mikoa yote na utadumu kwa majuma manne hadi katikati ya mwezi Januari mwakani," alisema meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud alipoongea na waandishi jana.

"Mgawo utahusisha mikoa yote iliyounganishwa kwenye gridi ya taifa isipokuwa mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Kigoma, Lindi na Mtwara."

Kwa mujibu wa Masoud, mgawo wa sasa umetokana na upungufu wa umeme uliojitokeza baada ya moja ya visima vinavyozalisha gesi vya kampuni ya Pan African Energy, kuzimwa.
Alisema kisima hicho kinachotoa gesi kimezimwa kwa ajili ya kukifanyia matengenezo ya kawaida, hivyo kusababisha upungufu wa megawati 40 za umeme zinazokwenda katika gridi ya taifa.

Pan African Energy ni kampuni ambayo inachimba gesi hiyo eneo la Songo Songo, Kilwa na baadaye husafishwa na kusafirishwa na kampuni ya Songas ambayo huzalisha umeme wa megawati 180 eneo la Ubungo na kuiuzia Tanesco.

Kwa mujibu wa makubaliano, Songas hutakiwa kuzalisha umeme kwa kiwango kilicho kwenye mkataba na ni jukumu la Tanesco kuutumia umeme huo wa gesi kulingana na mahitaji yake au kutoutumia. Tanesco huilipa Songas hata pale inapokuwa haitumii umeme wa kampuni hiyo.

Badra alisema kuwa kiwango hicho cha upungufu wa umeme kinaweza kuongezeka hadi kufikia megawati 120 jambo alilosema likitokea, shirikma hilo litazidisha mgawo.
“Wakati mwingine kunapokuwa na peak (matumizi yanakuwa makubwa), upungufu unaweza kufikia megawati 120. Ikitokea hivyo, kwa kuwa sasa tunategemea uzalishaji umeme kwa njia ya maji, itabidi nasi tuongeze mgawo,” alisema Badra.

Alieleza kuwa mgawo huo utaanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni katika baadhi ya maeneo huku maeneo yaliyopata umeme katika muda huo yakiukosa kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku mara tatu kwa wiki.

Kwa mujibu wa Badra, ratiba ya mgawo huo zitatangazwa katika magazeti na vyombo vingine vya habari.
Hata hivyo, alisema baadhi ya maeneo hayatakumbwa na mgawo huo akitaja baadhi kuwa ni hospitali, pampu za maji, migodi na viwandani ambako alisema vitakosa umeme usiku ili mchana viendelee kuzalisha.

Alisema kuwa maeneo yanayopata umeme kutoka transoma ya Kipawa hawatakumbwa na mgawo huo, kutokana na kukamilika kwa matengenezo yake.

“Transfoma ya Kipawa imeshatengemaa na hivyo kuanzia Desemba 23 (jana) haki ya kupata umeme katika maeneo yaliyoathirika kutokana na kuharibika kwa transfoma hiyo, itarejea kama kawaida na wateja wa maeneo hayo hawatakumbwa na mgawo huu tulioutangaza,” alisema Badra.

Baadhi ya maeneo yanayopata umeme kutoka transfoma hilo ni pamoja na Yombo Dovya, Tandika, Temeke, Chang’ombe, Chamazi, Tazara, Maji Matitu, Charambe, Keko na Uwanja wa Taifa.

Akizungumzia siku kuu za Krisimasi na Mwaka Mpya, Badra alisema Tanesco itajitahidi kuhakikisha wananchi wanasherehekea siku hizo bila kukosa umeme huku akiwaomba radhi kwa mgawo huo.

Mgawo wa umeme, ambao ulizalisha kashfa kubwa ya Richmond ulipoibuka mwaka 2006, umeshaanza kuzoeleka kwa wananchi na ahadi za shirika hilo na wizara kugeuza tatizo hilo kuwa historia, sasa zinaonekana za kawaida.

Machi 16 mwaka huu Tanesco ilitangaza mgawo wa umeme katika mikoa yote ya Tanzania Bara uliokuwa wa saa tano kila siku. Wakati mgawo huo ukiisha, Tanesco ilitangaza kuwa tatizo la umeme sasa litakuwa historia.

Watanzania, ambao ni asilimia 12 tu wanaotumia huduma hiyo majumbani, pia walipata machungu ya mgawo wa umeme Oktoba mwaka uliopita ambapo walikosa huduma hiyo kwa saa 12 kwa siku.

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa shirika hilo Stephen Mabada, alitangaza mgawo huo akieleza kwamba Tanesco ililazimika kuanza mgawo huo kutokana na upungufu mkubwa wa uzalishaji umeme, uliosababishwa na kuharibika kwa mitambo minne kwenye vituo vya uzalishaji wa nishati hiyo.

Mitambo iliyoharibika ilikuwa ni ya Kidatu, mkoani Morogoro, Kihansi (Iringa) na Pangani (Tanga) wakati jijini Dar es Salaam mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia wa Songas pia uliripotiwa kuharibika.

Wakati huo, serikali iliamuru kuwashwa kwa mitambo inayozalisha umeme kwa kutumia mafuta ya IPTL licha ya kampuni hiyo na Tanesco kuwa kwenye mgogoro mkubwa ambao unashughulikiwa mahakamani.

Matatizo makubwa ya umeme yaliibuka mwaka 2006 wakati nchi ilipokumbwa na janga kubwa la ukame na ikabidi serikali ichukue hatua za dharura kumaliza tatizo hilo.

Lakini hatua hizo za dharura zikaishia kwenye kashfa kubwa ya utoaji zabuni ya uzalishaji umeme kwa kampuni ya Richmond Development LLC, ambayo ilidhihirika baadaye kuwa haikuwa na uwezo wa kutekeleza wajibu wake kwenye mkataba.

Baadaye mkataba huo ulirithishwa kwa kampuni ya Dowans Tanzania ambayo, licha ya kuchelewa, ilileta nchini mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi iliyokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 120.

Lakini mwaka 2008 Tanesco ilikatisha mkataba huo mwaka mmoja kabla ya kumalizika, ikidai kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ilikiukwa wakati wa kuingia mkataba huo, lakini ikaahidi kuwa ina uwezo wa kuzalisha umeme bila ya kutegemea jenereta hizo.

Uamuzi huo uliifanya Dowans kufungua kesi Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), ikidai kuwa taratibu hazikufuatwa wakati wa kuvunja mkataba huo.

Mwaka mmoja baadaye Tanesco ikaibuka na hoja ya kutaka kuinunua mitambo hiyo ya Dowans, ikidai kuwa nchi ilikuwa hatarini kuingia kwenye tatizo kubwa la umeme na kwamba isingekuwa rahisi kununua mitambo mingine kabla ya tatizo hilo kuanza.

Hata hivyo, hoja hiyo ilipingwa vikali na Kamati ya Madini na Nishati ambayo ilieleza kuwa kununua mitambo hiyo mitumba ni kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma, kitu kilichomfanya mkurugenzi wa Tanesco wa wakati huo, Dk Idris Rashid kutoa tamko kuwa iwapo nchi itaingia gizani, asilaumiwe.

Mapema mwezi huu, ICC) ilitoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Dowans na kuiamuru Tanesco kuilipa kampuni hiyo binafsi fidia ya Sh185 bilioni.

Source: www.mwananchi.co.tz
Posted by Safari at Saturday, December 25, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Thursday, December 23, 2010

Use... this... in... Life

Talk---------------Softly
Walk----------------Humbly
Eat-------------------Sensibly

Breathe--------------------Deeply
Sleep----------------------Sufficiently
Dress---------------------------Smartly
Act-------------------------------Fearlessly
Work---------------------------------Patiently
Think-----------------------------------Truthfully
Believe------------------------------------Correctly
Behave-----------------------------------------Decently
Learn---------------------------------------------Practically
Plan-----------------------------------------------------Orderly
Earn----------------------------------------------------------Honestly
Save--------------------------------------------------------------Regularly
Spend---------------------------------------------------------------Intelligently
Love---------------------------------------------------------------------Passionately

Posted by Safari at Thursday, December 23, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Importance of having Breakfast:

Breakfast can help prevent strokes, heart attack and sudden death.
Advice on not to skip breakfast!
Tips for healthyliving...

For those who always skip breakfast, you should start kicking that habit now!!
You've heard many times that "Breakfast is the most important meal of the day."

Now, recent research confirms that one of the worst practices you can develop may be avoiding breakfast.


Why?

Because the frequency of heart attack, sudden death, and stroke peaks
between
6:00a.m. and noon, with the highest incidence being between 8: 00a.m. and 10:00a.m.What mechanism within the body could account for this significant jump in sudden death in the early morning hours? :-(

We may have an answer .

Platelet, tiny elements in the blood that keep us from bleeding to Death if we get a

cut, can clump together inside our arteries due to cholesterol or laque buildup in the

artery lining. It is in the morning hours that platelets become the most activated and

tend to form these internal blood clots at the greatest frequency.

However, eating even a very light breakfast prevents the morning platelet activation that is associated with
heart attacks and strokes . :-)
Studies performed at Memorial University in St.Johns, Newfoundland found that
eating a light, very low-fat breakfast was critical in modifying the morning platelet

activation. Subjects in the study consumed either low-fat or fat-free yogurt, orange

juice, fruit, and a source of protein coming from yogurt or fat-free milk.

S o if you skip breakfast, it's important that you change this practice immediately
in light of this research.Develop a simple plan to eat cereal, such as oatmeal or Bran

Flakes ,along with six ounces of
grape juice or orange juice , and perhaps a piece of
fruit
.
This simple plan will keep your platelets from sticking together, keep blood clots
from forming, and perhaps head off a potential heart attack or stroke.

So never ever skip breakfast :-)

FORWARD THE MESSAGE TO YOUR
COLLEAGUES.

for educating the community.

Posted by Safari at Thursday, December 23, 2010 2 comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Sunday, December 19, 2010

Please read and pass on. This could happen to you or your loved ones.

A man came over and offered his services as a painter to a lady who
was buying petrol at a filling station. He gave her his "complimentary
card".
She said "No", but after some persuasion, she accepted his card out of
kindness and got in her car.

The man then got into a car driven by another gentleman..

As the lady left the service station, she saw the men following her
out of the station at the same time.

After driving a short distance, she started feeling dizzy and could
not catch her breath. She tried to open the window and realized that
her hand had a sweet smelling odour. This was the same hand she used
to acce pt the card from the gentleman at the Petrol station.

She then noticed the men were trailing her. Their car was immediately
behind her and she knew she had to do something at that moment. She
drove into the first turning on her right and it was a busy road. She
began to honk her horn repeatedly, non- stop and started shouting for
help.

She stopped her car and continued horning and within a few minutes,
her car was surrounded by a crowd.

On seeing the situation, the men drove away, but the lady still felt
bad for several minutes. She was able to tell the crowd her husband's
GSM phone number and somebody in the crowd called him. He arrived, the
scene and took her to a high brow hospital for treatment. She was
discharged after 48 hours.

WHAT HAPPENED?

Apparently, there was a substance on the card that could have
seriously injured her. This drug is called 'BURUNDANGA' and it is used
by CRIMINALS who wish to inca pacitate a victim in order to steal, kill
or take advantage of women (RAPE).

This drug is 4times more dangerous than the date rape drug and it is
transferable on simple cards and papers.

So take heed and make sure you don't accept cards at any given time
(when you are alone) from STRANGERS - in the streets, markets, filling
stations etc. This applies to those making house calls and slipping
you a card when they offer their services.

Don't be caught unawares.

Be vigilant

Be prayerful - tell God to sharpen your Gut instincts.

Be bold and say NO when you are not convinced.

Don't be emotional when dealing with strangers.

Don't be ashamed to scream and shout on top of your voice when you are
in danger.

Don't keep late nights.

Please send this email alerts to all your friends both MALE & FEMALE you may just save a LIFE.
Posted by Safari at Sunday, December 19, 2010 1 comment:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Difference Between Complete & Finish... :)


People say there is no difference between COMPLETE & FINISH...

But there is.

When you marry the right one, you are COMPLETE ....

And when you marry the wrong one, you are FINISHED .....

!

!

!

!

!

!

And when the right one catches you with the wrong one, you are ...


COMPLETELY FINISHED !

------

Posted by Safari at Sunday, December 19, 2010 1 comment:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Saturday, December 18, 2010

mambo ya gado
Posted by Safari at Saturday, December 18, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
BREKING NYUUUUZZZZZ: ABOU SEMHANDO WA TWANGA PEPETA AFARIKI AJALINI DAR
Marehemu Abou Semhando 'Baba Diana' enzi za uhai wake. Hapo ilikuwa katika show ya Old Skul viwanja vya Karimjee ambapo wakongwe wa muziki walikusanyika kutumbuiza
Marehemu Abou Semhando (kulia, fulana nyekundu) akiwa katika mazishi ya Dk. Remmy Ongala na wakongwe wenzie. Toka shoto ni Mzee Makassy, Tschinga Kalala Assosa, King Kikii na Kanku Kelly
Pikipiki ya Marehemu Abou Semhando baada ya kupata ajali
Gari linalosadikiwa kuhusika na ajali hiyo likiwa mtaroni

Na John Kitime

Katika hali ya kusikitisha nalazimika kutaarifu kuwa mwanamuziki mwingine wa zamani, Abou Semhando ambaye ni mpiga drums wa miaka mingi amefariki dunia mida ya saa tisa usiku, alfajiri ya Jumamosi 18 December 2010, katika ajali ya pikipiki yake kugongwa na gari.

Marehemu Abou Semhando, maarufu kwa jina la 'Baba Diana', pia alikuwa mmoja wa waasisi na viongozi waandamizi wa The Affrican Stars 'Twanga Pepeta' kabla ya umauti kumfika. Bendi zingine alizopigia wakati wa uhai wake ni pamoja na Sola TV, Vijana Jazz na Super Matimila.


Katika ajali hiyo gari aina ya benzi imegonga nyuma pikipiki yake wakati akitoka kupiga mziki maeneo ya Africana. Alipiga drums nyimbo ya pili toka mwisho na kuelekea nyumbani ambapo ndipo alipokutana na ajali hiyo.


Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa Abou alikuwa mmoja ya waliokuwa wakitangulia mbele ya msafara wa mazishi ya Remmy Ongala na pikipiki yake.
Posted by Safari at Saturday, December 18, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
TOLEO LA NOTI MPYA

  1. Benki kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la noti za shs 500, 1000, 2000, 10,000. Noti hizi zitaingizwa katika mzunguko tarehe 1 Januari 2011. Noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya. Zitaendelea kutumika na kuwepo katika mzunguko sambamba na hili toleo jipya la noti mpaka hapo hizo za zamani zitakapotoweka taratibu na hatimaye kwisha kabisa kwenye mzunguko. Hivyo basi, wananchi wanashauriwa kuendelea kuzipokea na kuzitumia noti za zamani bila shaka au wasiwasi wowote kuhusu uhalali wake hadi hapo zitakapokwisha na kutoweka kabisa katika mzunguko. Vilevile ieleweke kuwa hakutakuwa na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa mpya.

  1. Toleo hili la noti mpya lina taswira inayozingatia mandeleo ya uchumi na jamii. Tumefanya mabadiliko kidogo katika toleo jipya kwa kuweka picha za waasisi wa taifa letu. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaonekana kwenye noti ya shilingi elfu moja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwenye noti ya shilingi mia tano. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, elfu tano na elfu kumi zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama. Hata hivyo, kutokana na kupunguza ukubwa wa noti hizi mpya tumeweka picha za vichwa vya wanyama hao badala ya wanyama wazima kama ilivyo kwenye noti za zamani.

  1. Ili kupambana na uhalifu wa kughushi na kuongeza muda wa noti hizi kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu kabla ya kuchakaa, toleo hili limeongezewa ubora kwa kuweka alama maalum mpya za usalama na kutumia taaluma mpya ya kuziimarisha. Alama mbali mbali za usalama zimeboreshwa na kwa mara ya kwanza kabisa alama ya “motion” ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho imetumika katika noti hizi. Ili kuelimisha wananchi kuhusu alama za usalama zinazotambulisha uhalali wa noti zetu, tumetoa matangazo na vipeperushi ambavyo vitasambazwa sehemu mbali mbali za nchi. Taarifa ya alama za usalama za noti pia zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu kwa anwani www.bot-tz.org

  1. Ni muhimu kwa umma kufahamu alama za usalama ili uweze kutofautisha noti halali na bandia kwa urahisi. Hata hivyo Benki Kuu inapenda kutahadharisha watu wawe waangalifu na kuzichunguza noti zote wanazopokea hasa kwenye giza ili kuhakikisha kwamba ni noti halali. Uchunguzi ufanywe kwa noti zote zilizopo kwenye mzunguko pamoja na za zamani. Endapo wana mashaka warejee kwenye mabango na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu au tawi lolote la Benki Kuu.

Gavana

Benki Kuu ya Tanzania


Posted by Safari at Saturday, December 18, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

Friday, December 17, 2010

Gavana wa Benki kuu azindua noti mpya leo
Posted by Safari at Friday, December 17, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
waziri mkuu aongea na wahariri leo
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akisisitiza jambo katika mkutano wake na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake mjini Dar es salaam
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akiongea na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake mjini Dar es salaam leo.Picha zote na Anna Itenda - MAELEZO
Posted by Safari at Friday, December 17, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
SAFARI YA MWISHO YA DR.REMMY ONGALA ILISINDIKIZWA NA UMATI WA WATU



Picha zote kwa hisani ya: Bongo Celebrity

PUMZIKA KWA AMANI
Posted by Safari at Friday, December 17, 2010 No comments:
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest
Newer Posts Older Posts Home
Subscribe to: Posts (Atom)

East African Time

Safari Dennis.

Maoni/Salamu !!


Karibuni sana kwa kuangalia na Maoni.

Haya jamani msisite kutuma maoni na maswala yoyote yanayohusu jamii kwa kutumia mail yangu safari2tz@gmail.com

Kwa ajili ya kuangalia site nyingine !!

  • CULINARY CHAMBER
  • Hisapepe
  • Magari yanayouzwa Tanzania
  • Tanzania real estate
  • www.mactemba.blogspot.com
  • www.mazingirachanya.blogspot.com
  • www.zachariahtz.blogspot.com

Blog Mnaionaje ?

Total Pageviews

Load Counter
obagi

Followers

Kutafuta site mbali mbali

Karibu ujionee Tanzania yetu na Dunia kwa ujumla.

Endelea

Habari zilizopo.

  • ►  2014 (4)
    • ►  September (1)
    • ►  July (1)
    • ►  March (2)
  • ►  2013 (10)
    • ►  December (1)
    • ►  February (6)
    • ►  January (3)
  • ►  2012 (110)
    • ►  December (2)
    • ►  October (1)
    • ►  September (27)
    • ►  August (19)
    • ►  July (17)
    • ►  June (20)
    • ►  May (6)
    • ►  February (1)
    • ►  January (17)
  • ►  2011 (177)
    • ►  December (4)
    • ►  September (1)
    • ►  July (4)
    • ►  June (12)
    • ►  May (25)
    • ►  April (35)
    • ►  March (18)
    • ►  February (16)
    • ►  January (62)
  • ▼  2010 (384)
    • ▼  December (28)
      • EXCLUSIVE INTERVIEW WITH SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI...
      • Tangazo !!Kwa yule anaehitaji nyumba maeneo ya sin...
      • BREAKING NYUUUZZZZ:CHENGE AFANIKIWA KUKWEPA LUPANG...
      • AU YAMTAKA RAILA KUSULUHISHA MGOGORO WA IVORY COA...
      • BREAKING NEWS…!!! Risasi zinarindima katika Mae...
      • WANANCHI AUSTRALIA WAKIMBIA MAFURIKO KATIKA JIMBO...
      • Bagamoyo panazidi kupendeza. ...
      • MSAADA TUTANI
      • FFU wa Ngoma Africa Band Kukiwasha nchini Serbia 2...
      • Marehem Hassan Jumanne Makunja Amezaliwa 4-03-196...
      • JOKE!!A three-year-old wal...
      • Balance sheet of life ...
      • TangazoKwa wale wanaohitaji Nyumba ya kupanga!!Kun...
      • Jeshi la Magereza Sasa Kujiendesha Kisayansi ...
      • Wapenzi wa blog hii ya Inawezekana Nawatakia xmass...
      • NYOTA WANAOTAMBA BONGO KWA SASA ...
      • Tanesco yatangaza mgawo wa umeme nchi nzima ...
      • Use... this... in... Life Talk---------------Soft...
      • Importance of having Breakfast: Breakfast ...
      • Please read and pass on. This could happen to you ...
      • Difference Between Complet...
      • mambo ya gado
      • BREKING NYUUUUZZZZZ: ABOU SEMHANDO WA TWANGA PEPET...
      • TOLEO LA NOTI MPYA ...
      • Gavana wa Benki kuu azindua noti mpya leo ...
      • waziri mkuu aongea na wahariri leo ...
      • SAFARI YA MWISHO YA DR.REMMY ONGALA ILISINDIKIZWA...
      • kushinda mitihani ni kanziJamaa watatu walikuwa...
    • ►  November (11)
    • ►  October (21)
    • ►  September (33)
    • ►  August (34)
    • ►  July (34)
    • ►  June (43)
    • ►  May (17)
    • ►  April (16)
    • ►  March (73)
    • ►  February (61)
    • ►  January (13)
  • ►  2009 (527)
    • ►  December (63)
    • ►  November (13)
    • ►  October (16)
    • ►  September (82)
    • ►  August (34)
    • ►  July (80)
    • ►  June (37)
    • ►  May (58)
    • ►  April (19)
    • ►  March (67)
    • ►  February (28)
    • ►  January (30)
  • ►  2008 (2137)
    • ►  December (127)
    • ►  November (80)
    • ►  October (217)
    • ►  September (229)
    • ►  August (293)
    • ►  July (363)
    • ►  June (290)
    • ►  May (172)
    • ►  April (222)
    • ►  March (144)
Awesome Inc. theme. Theme images by mammamaart. Powered by Blogger.